Tuesday 31 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Fainali ya FA Cup yazua utata!
Chama cha Soka cha England, FA, na Wasimamizi wa Ligi Kuu wanahaha kutafuta ufumbuzi wa lini Fainali ya Kombe la FA ichezwe ili isigongane na Mechi za mwisho mwisho za Ligi.
Utata wa Fainali hiyo ya Kombe la FA umezuka kwa sababu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI itachezwa Mei 28 Uwanjani Wembley Jijini London ambako pia Fainali ya FA Cup huchezwa.
Na ili ukubaliwe kuwa Mwenyeji wa Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI ni lazima uhakikishe Kiwanja kitakachochezewa Fainali hiyo hakichezwi Mechi yeyote kwa Wiki mbili kabla ya Fainali hiyo ili kukiandaa vyema.
Sharti hilo linamaanisha Fainali ya FA Cup itabidi ichezwe Mei 14 wakati Mechi za Mwisho za Ligi Kuu zinachezwa Mei 22.
Kawaida Fainali ya Kombe la FA huchezwa Wiki moja baada ya Ligi Kuu kumalizika.
Ni mara moja tu Fainali hiyo ilichezwa Wiki moja kabla Ligi Kuu kumalizika na hiyo ilikuwa Msimu wa Mwaka 2000/1.
Utata huu pia umechangiwa na kuihamisha Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI kutoka kuchezwa Siku ya Jumatano na kupelekwa Jumamosi utaratibu ambao ulianza Msimu uliokwisha.
FA imetamka itakaa chini na Wasimamizi wa Ligi Kuu ili kutoa ufumbuzi wa utata huo.
Werder Bremen yamchukua Silvestre
Mchezaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Mikael Silvestre amejiunga na Klabu ya Ujerumani German Werder Bremen kwa Mkataba wa Miaka miwili.
Silvestre amejiunga Bremen kama Mchezaji huru baada ya Mkataba wake na Arsenal kumalizika Mwezi Juni.
Silvestre, Miaka 33, alieichezea Timu ya Taifa ya Ufaransa mara 40, alianza Soka la Kulipwa huko Ufaransa na Klabu ya Rennes na kuhamia Inter Milan kisha Manchester United Mwaka 1999 alikokaa hadi 2008 na kujiunga na Arsenal.
Kocha wa Bremen Thomas Schaaf amesema Silvestre ni hazina kwa Wachezaji Chipukizi na bado anao uwezo wa kutoa mchango mkubwa kwa Klabu hiyo.

No comments:

Powered By Blogger