Sunday, 29 August 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Bolton 2 Birmingham 2
Mtu 10 Bolton Wanderers walipigana kutoka bao 2-0 nyuma na kufanya gemu imalizike 2-2 Uwanjani kwao Reebok.
Birmingham walipata bao la kwanza dakika ya 3 tu kupitia Roger Johnson kufuatia krosi kutoka kushoto.
Kipa wa Bolton, Jussi Jaaskelainen, alitolewa kwa Kadi Nyekundu muda mfupi kabla ya haftaimu kwa kumnasa kibao Roger Johnson.
Kipindi cha pili, dakika ya 50, Craig Gardner akafunga bao la pili kwa Birmingham.
Bolton walifunga bao lao la kwanza dakika ya 71 kwa penalti Mfungaji akiwa Kevin Davies na Robbie Blake akasawazisha kwenye dakika ya 81 baada ya frikiki nzuri sana.
Liverpool wamchota Meireles wa Porto
Liverpool imemsaini Kiungo wa Kimataifa wa Ureno, Raul Meireles, kutoka FC Porto kwa dau la Pauni Milioni 11.5 na amesaini Mkataba wa Miaka minne.
Meireles, ambae alicheza Mechi zote za Ureno huko Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia, amechukuliwa kama mbadala wa Kiungo Javier Mascherano alieondoka Liverpool kwenda Barcelona.
Msimu huu Liverpool, pamoja na Meireles, Wachezaji wengine wapya waliosajiliwa ni Milan Jovanovic, Joe Cole, Christian Poulsen, Jonjo Shelvey na Danny Wilson.
Ferguson amsifia Rooney
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amemsifia Straika wake Wayne Rooney baada ya kuumaliza ukame wa magoli alipofunga bao la kwanza kwa penalti katika ushindi wa 3-0 dhidi ya West Ham katika Mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa Old Trafford hapo jana.
Ferguson amesema: ‘Mastraika siku zote wana uchu wa kufunga lakini tuzungumzie uchezaji wa Rooney. Yeye anajituma mno uwanjani.”
Licha ya kufunga bao moja, Rooney pia ndie alielipika bao moja la Man United kati ya mengine mawili yaliyofungwa.
Kwa vile Ligi Kuu inasimama hadi Septemba 11 kupisha Mechi za Kimataifa za Nchi za Ulaya kuwania kufuzu Fainali za EURO 2012, Rooney anategemewa kujiunga na Timu ya England ambayo Ijumaa Septemba 3 itacheza na Bulgaria na kisha Jumanne Septemba 7 kucheza na Uswisi.

No comments:

Powered By Blogger