Friday 16 May 2008

FAINALI YA KOMBE LA F.A

JUMAMOSI, 17 MEI 2008=

PORTSMOUTH vs CARDIFF CITY
saa 11 jioni [bongo time]

Kesho ndio fainali ya 'vibonde' itakayochezwa WEMBLEY STADIUM ikizikutanisha timu ambazo si vigogo!
Wengi wanawajua wachezaji wa Portsmouth kwani wanawaona mara kwa mara katika mechi za LIGI KUU.
Wachezaji hao kama Kanu, Sule Muntari, Sol Campbell, David James n.k wanategemewa kushuka uwanjani kwa timu ya Portsmouth.
Jermaine Defoe ambae alitokea Tottenham Hotspurs mwanzoni mwa mwaka haruhusiwi kuichezea Potsmouth katika fainali hii kwani alishacheza mechi za F.A msimu huu akiwa na SPURS.
Wachezaji wa CARDIFF CITY ambao ni maarufu kwetu bila shaka watakuwa ni maveterani ROBBIE FOWLER na JIMMY FLOYD HASSELBAINK.
REFA KATIKA PAMBANI HILO ATAKUWA MIKE DEAN.
MIKE DEAN amechezesha mechi 28 za LIGI KUU msimu huu na ametoa KADI NYEKUNDU 9 na za NJANO 106.
================================================================================

No comments:

Powered By Blogger