Thursday 15 May 2008



RANGERS [SCOTLAND] 0 ZENIT ST PETERSBURG 2!


Timu ya ZENIT YA URUSI imenyakua Kombe la UEFA hapo jana baada ya kuifunga RANGERS YA SCOTLAND mabao 2-0 katika fainali iliyochezwa UWANJA WA MANCHESTER CITY uitwao CITY OF MANCHESTER STADIUM.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RONALDO NA MENEJA WAKE, SIR ALEX FERGUSON WAPATA TUZO ZA JUU!!!

Ronaldo ameshinda tuzo ya MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU UINGEREZA na pia amenyakua KIATU CHA DHAHABU baada ya kuwa MFUNGAJI BORA katika ligi hiyo baada ya kupachika jumla ya mabao 31.
Hii ni mara ya kwanza tangu miaka 12 iliyopita kwa mcheza ji kufunga zaidi ya mabao 30 wakati ALAN SHEARER, akichezea BLACKBURN wakati huo nae alipofunga magoli 31.
NAE ALEX FERGUSON AMENYAKUA TUZO YA MENEJA BORA WA MSIMU HII IKIWA NI MARA YA 8 KWAKE.
FERGUSON ameshatwaa UBINGWA WA LIGI KUU MARA 10 na KOMBE LA FA MARA 5,.
************************************************************************************************
TIMU YA TATU KUPANDA LIGI KUU UINGEREZA
HULL CITY 4 WATFORD 1

Timu ya HULL CITY itapambana na BRISTOL CITY katika fainali itakayoamua timu ipi itaungana na WEST BROMWICH ALBION na STOKE CITY kupanda daraja na kwenda LIGI KUU UINGEREZA.
HULL CITY, hapo jana, iliifunga WATFORD mabao 4-1. Katika mechi ya kwanza HULL CITY ilishinda mabao 2-0.


No comments:

Powered By Blogger