Friday 16 May 2008

SAMMY LEE ARUDI LIVERPOOL!!!
Mchezaji nyota wa zamani wa LIVERPOOL, SAMMY LEE, amerudi tena LIVERPOOL na kuteuliwa kuwa MENEJA MSAIDIZI chini ya uongozi wa MENEJA wa sasa RAFAEL BENITEZ.
SAMMY LEE alikuwa kiungo nyota na mahiri wa timu ya LIVERPOOL iliyong'ara na kuwika katika miaka ya 1980.
Baada ya kustaafu uchezaji hapo LIVERPOOL, SAMMY LEE aliteuliwa kwenye timu hiyohiyo kuwa MENEJA wa TIMU YA AKIBA na baadae akafanya kazi chini ya MAMENEJA waliofuatia wa LIVERPOOL, GRAEME SOUNESS na GERARD HOULLIER.
Mwaka 2004, alifanya kazi kama mmoja wa Makocha wa Timu ya Taifa ya UINGEREZA na kisha 2005 alienda BOLTON kuwa msaidizi wa SAM ALLARDICE.
=====================================================================

No comments:

Powered By Blogger