Friday 10 October 2008

NAHODHA WA ENGLAND JOHN TERRY HUENDA ASICHEZE JUMAMOSI!

Nahodha wa Timu ya Taifa John Terry huenda asicheze mechi ya Jumamosi dhidi ya Kazakhstan ya Kundi la 6 la Nchi za Ulaya ya mitoano ya Kombe la Dunia kuwania nafasi za kuingia Fainali zitazochezwa Afrika Kusini mwaka 2010 kwa sababu anaumwa mgongo.
John Terry hakufanya mazoezi ya Timu ya England hapo jana na nafasi yake kwenye mechi hiyo huenda ikachukuliwa na mmoja kati ya Matthew Upson, Wes Brown au Joleon Lescott.
Endapo hatocheza basi Unahodha wakati wa mechi utachukuliwa na Rio Ferdinand ambae ni Naibu Nahodha wa England.

FLETCHER ATEULIWA NAHODHA SCOTLAND

Nae Mchezaji mwenzake Rio Ferdinand kwenye Klabu ya Manchester United, Darren Fletcher ameteuliwa kuwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Scotland kwenye mechi ya Jumamosi dhidi ya Norway ya mitoano ya kuwania nafasi za kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwaka 2010.
Darren Fletcher amechukua nafasi ya Nahodha wa siku zote Barry Ferguson ambae ameumia enka na Naibu wake Stephen McManus amefungiwa mechi kwa kuwa na adhabu ya kadi.
Darren Fletcher, mwenye umri wa miaka 24, ni mara ya nne kuteuliwa kuwa Nahodha wa Nchi yake Scotland.

No comments:

Powered By Blogger