Monday 6 October 2008

KWA MAPENZI YA EVERTON, AMPACHIKA BINTI YAKE KICHANGA JINA EVA-TONI-ANN: ukilitamka unamaanisha wewe ni shabiki wa kutupwa wa EVERTON!!!

Kabinti kachanga kilichozaliwa ndani ya Familia ya Mashabiki wenda wazimu wa Klabu ya Everton iliopo jijini Liverpool huko Uingereza kilijikuta kikibatizwa majina matatu yaliyounganishwa yaani EVA-TONI-ANN na ukiyatamka basi unakuwa unataja EVERTONIAN na hiyo inamaanisha wewe ni Shabiki wa kutupwa wa Klabu ya Everton!
Baba mtoto huyo EVA-TONI-ANN aitwae Danny Pierce amesema hiyo ilikuwa ndoto yake tangu yuko mtoto shuleni alipoapa akipata binti basi atampa majina hayo kuonyesha mapenzi thabiti kwa Timu yake Everton.
Lakini ndoto hiyo haikutimia pale alipozaa watoto wawili wa kike wa kwanza na mkewe Bibi Claire Cooper aligomea jina hilo la Eva-Toni-Ann.
Lakini baada ya kukerwa sana na mumewe, Claire alikiri jina hilo lilianza kumwingia akilini ingawa alikuwa bado halipendi.
Pale alipozaliwa binti huyo mpya ikapigwa kura.
Wakaandika majina tofauti kwenye karatasi na kuvitia vikaratasi hivyo ndani ya kofia likiwemo lile la Eva-Toni-Ann.
Baba mtu Danny akatoa karatasi ndani ya kofia na liliposomwa jina lilikuwa ni Eva-Toni-Ann! Ilipokuja zamu ya Binti yao wa kwanza kuokota karatasi ndani ya kofia hiyo likatoka jina Eva-Toni-Ann!
Mamu mtu nae ilipofika zamu yake jina likawa hilo hilo Eva-Toni-Ann!
Baba wa mtoto huyo Eva-Toni-Ann anakiri kama angezaliwa dume basi angemwita Duncan- akimaanisha Duncan Ferguson aliyekuwa Mchezaji veterani na mahiri wa Everton.

Danny anasema hata Babu yake mtoto huyo Eva-Toni-Ann alikuwa ni mpenzi wa Everton na alifurahia jina hilo ingawa hakuishi muda mrefu tangu azaliwe mjukuu wake kwani alifariki kwa kuungua moto nyumbani kwake!

Danny anakiri hata Mashabiki wa Watani wao Klabu ya Liverpool wanakiri jina hilo ni maridadi sana!

No comments:

Powered By Blogger