Monday, 6 October 2008

MITOANO KOMBE LA DUNIA: KUNDI LA NCHI ZA MAREKANI KUSINI NA RATIBA YAO YA WIKIENDI HII

Timu za Taifa za Nchi za Marekani Kusini zinaingia tena dimbani kuanzia Jumamosi hii katika mapambano ya Kundi lao ambalo lina Nchi 10. Mpaka sasa kila Nchi ishacheza mechi 8 na ikifika Jumatano ya tarehe 15 Oktoba 2008 watakuwa wameshavuka nusu ya mechi wanazotakiwa kucheza na hivyo kuleta picha kidogo nani anaweza akaingia FAINALI huko AFRIKA KUSINI mwaka 2010.

Baada ya mechi 8 kwa kila timu, Paraguay yuko kileleni akiwa na pointi 17 akifuatiwa na Brazil mwenye pointi 13 sawa na Argentina na Chile lakini Brazil yuko mbele kwa kufunga magoli mengi. Uruguay ana pointi 12, Colombia 10, Ecuador 9, Venezuela na Peru wana 7 kila mmoja na mkiani yuko Bolivia mwenye 5.
Timu nne za juu za Kundi hili zitaingia moja kwa moja FAINALI huko AFRiKA KUSINI mwaka 2010.

Timu ya 5 itakwenda kupambana na mshindi wa Kundi la Oceania ili kupata timu moja kati ya hizo itakayoingia FAINALI hizo.

RATIBA:

Jumamosi 11 Oktoba 2008

Bolivia v Peru

Argentina v Uruguay

Colombia v Paraguay


Jumapili 12 Oktoba 2008

Venezuela v Brazil

Ecuador v Chile

Jumanne 14 Oktoba 2008

Bolivia v Uruguay


Jumatano 15 Oktoba 2008

Paraguay v Peru

Chile v Argentina

Venezuela v Ecuador

Brazil v Colombia

No comments:

Powered By Blogger