WWW.SOKAINBONGO.COM

Wadau,
Tuko mbioni kutengeneza Tovuti www.sokainbongo.com ambayo itakuwa na kila habari za soka zikiwemo pia za bongo.
Tunakaribisha maoni, mawaidha na michango yenu ili kufanikisha uandaaji na utengenezwaji wa hiyo tovuti.
Shukran,
stormingfohadi

Wednesday, 11 November 2009

Hargreaves njiani kurudi dimbani!!!
Mchezaji mahiri na kiraka wa Manchester United, Owen Hargreaves, yuko njiani kuonekana tena uwanjani baada ya kupona matatizo ya magoti na yupo kwenye mazoezi makali.
Hargreaves amekuwa nje ya Uwanja kwa miezi 14 sasa tangu aumie Septemba, 2008 kwenye mechi na Chelsea ya dro 1-1 huko Stamford Bridge na ikabidi afanyiwe upasuaji kwenye magoti yake yote mawili.
Hargreaves amesema: “Nikirudi Uwanjani Old Trafford nitajisikia furaha na naweza kuzimia kwa furaha! Nataka nirudi nilipe fadhila kwa Mashabiki waliokuwa na imani na mimi!”
Real yabwagwa nje Copa del Rey!!!
Timu ya Kijijini inayocheza Daraja la chini huko Spain, Alcorcon, imeitupa nje ya mashindano kugombea Kombe la Mfalme Timu kubwa na tajiri Real Madrid licha ya jana Real kushinda 1-0 kwani Alcorcon waliibamiza Real 4-0 mechi ya kwanza.
Real walichezesha vigogo wao wote akina Raul, Kaka, Van Nistelrooy na wengineo lakini walishindwa kukomboa goli 4 na walipata kigoli chao kimoja mwishoni kupitia Rafael van der Vaart.
Mahasimu wa Real, Barcelona, wamesonga mbele kwenye Kombe hilo baada ya jana kushinda 5-0 dhidi ya Cultural Leonesa. Katika mechi ya kwanza, Barca walishinda 2-0.

0 comments:

Loading...