WWW.SOKAINBONGO.COM

Wadau,
Tuko mbioni kutengeneza Tovuti www.sokainbongo.com ambayo itakuwa na kila habari za soka zikiwemo pia za bongo.
Tunakaribisha maoni, mawaidha na michango yenu ili kufanikisha uandaaji na utengenezwaji wa hiyo tovuti.
Shukran,
stormingfohadi

Monday, 9 November 2009

FA yampa onyo Rooney kwa kauli: "MTU 12!! MTU 12!!' aliyoitoa baada ya mechi ya Chelsea jana!!!
Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney amepewa onyo na FA, Chama cha Soka England, na ametakiwa achunge mwenendo wake wa baadae baada ya kunaswa akipiga kelele kwenye Kamera ya TV 'MTU 12!! MTU 12!!', akimaanisha Refa kawabeba Chelsea,  mara tu baada ya mechi ya Ligi Kuu jana kumalizika huko Stamford Bridge kwa Chelsea kuifunga Man U 1-0 kwa goli la utata.
Pia FA imesema Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, hana hatia baada ya kutamka maamuzi ya Refa Martin Atkinson yalikuwa ni upuuzi wa hali ya juu na pia kusema maamuzi kama hayo yanawafanya watu wakose imani kwa Marefa. 
Kwa sasa Ferguson yupo matatani na FA akikabiliwa na kesi inayosubiri uamuzi baada ya kushitakiwa mwezi Oktoba pale alipodai Refa Alan Wiley hayuko fiti kuchezesha mara tu baada ya mechi kati ya Man U na Sunderland kwisha dro 2-2.

0 comments:

Loading...