Saturday 14 November 2009

Nigeria waipiku Tunisia na kutinga Fainali Kombe la Dunia!!
Mozambique 1 Tunisia 0
Kenya 2 Nigeria 3
Nigeria imefanikiwa kuipiku Tunisia pale ilipoifunga Kenya mabao 3-2 mjini Nairobi Uwanja wa Nyayo na Tunisia kutunguliwa 1-0 na Msumbiji mjini Maputo, Uwanja wa Machava.
Kenya ndio walitangulia kupata bao Mfungaji akiwa Dennis Oliech dakika ya 16.
Nigeria walisawazisha dakika ya 65 kupitia Obafemi Martins na Yakubu Ayegbeni akaweka la pili dakika 2 baadae.
Kenya wakasawazisha dakika ya 79 kupitia Wetende na matokeo yangebaki 2-2 hata kama Tunisia angefungwa huko Msumbiji basi Tunisia angefuzu.
Lakini alikuwa Obafemi Martins ndie alieipeleka Nigeria Fainali baada ya kupachika bao la 3 na la ushindi dakika ya 83.
Huko Maputo, uwanja wa Machava, Mchezaji wa Msumbiji Dario Monteiro, dakika ya 81, ndie aliewakata maini Tunisia kwa kufunga bao la ushindi.

No comments:

Powered By Blogger