Monday 9 November 2009

Ancelotti afurahia kumfunga “Mpinzani Bora!!!”
Carlo Ancelotti wa Chelsea amekiri kuwa amefurahishwa sana na kumfunga “Mpinzani Bora” baada ya Timu yake kuifunga Manchester United hapo jana kwenye Ligi Kuu Uwanjani Stamford Bridge bao 1-0.
Ingawa Chelsea walishinda kwa goli la utata lililolalamikiwa na Manchester United, mechi hiyo ilitawaliwa na Man U.
Ancelotti amesema: “Ilikuwa mechi ngumu! Kulikuwa hamna nafasi kwenye Kiungo, ilikuwa taabu kutengeneza nafasi! Sasa tuko pointi 5 mbele lakini inabidi tusilewe ushindi kwa kuifunga Timu Bora na Mpinzani wetu mkubwa!”
Wes Brown asisitiza Drogba alimchezea rafu Chelsea walipofunga goli!!
Rooney asikika akipiga kelele kwenye Kamera: “Mtu 12!! Mtu 12!!’
Mlinzi wa Manchester United Wes Brown amesisitiza kuwa Mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba alimchezea rafu wakati Chelsea wanafunga goli lao na Refa Martin Atkinson alipaswa kulikataa.
Chelsea walifunga goli lao dakika ya 76 kwa John Terry kupiga kichwa mpira wa frikiki ya Frank Lampard na mpira kumparaza Anelka, aliekuwa ofsaidi na kutinga wavuni.
Manchester United waliilalamikia frikiki hiyo kwa madai Darren Fletcher alicheza mpira na hakumgusa Ashley Cole aliejirusha.
Vilevile wamedai wakati Terry anapiga kichwa kufunga Drogba alimkamata na kumwangusha chini Brown.
Brown ametamka kwa masikitiko: “Sidhani Refa alichezesha vizuri! Lile goli si halali na hata frikiki ni utata mtupu! Lakini tutafanyaje ikiwa Refa haoni yote hayo?”
Mara baada ya mechi kwisha, mshambuliaji Nyota wa Manchester United Wayne Rooney alisikika akipiga kelele kwenye kamera: “Mtu 12!! Mtu 12!” bila shaka akimaanisha Refa alikuwa upande wa Chelsea.
Kikosi cha England kucheza na Brazil huko Doha, Qatar chatajwa!
Kocha wa England, Fabio Capello, amekitangaza Kikosi chake kitakachocheza mechi ya kirafiki na Brazil huko Doha, Qatar tarehe 14 Novemba 2009.
Katika Kikosi hicho wapo Darren Bent wa Sunderland ambae mara ya mwisho kuichezea England ni miezi 12 iliyopita kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Ujerumani na Beki wa Aston Villa, Stephen Warnock, ambae amechukuliwa badala ya Ashley Cole wa Chelsea anaesemekana kaumia.
Pia yupo Kiungo wa Tottenham, Tom Huddlestone, ambae ni mara ya kwanza kuitwa England.
Ingawa Beckham ametajwa kwenye Kikosi hicho lakini taarifa za baadaye zimesema hatowezi kujiunga na Timu kwa vile Klabu yake LA Galaxy ilishinda Nusu Fainali yake ya Ligi ya MLS hapo jana na hivyo kutinga Fainali.
Kikosi kamili ni: Foster (Manchester United), Green (West Ham), Hart (Manchester City); Bridge, Lescott (Manchester City), Brown (Manchester United), Cahill (Bolton), Johnson (Liverpool), Terry (Chelsea), Upson (West Ham), Warnock (Aston Villa); Barry, Wright-Phillips (Manchester City), Beckham (Los Angeles Galaxy), Carrick (Manchester United), Huddlestone, Jenas (Tottenham), Lampard (Chelsea), Milner, Young (Aston Villa); Bent (Sunderland), Crouch, Defoe (Tottenham), Rooney (Manchester United).

No comments:

Powered By Blogger