Sunday 8 November 2009

Fergie: “Tumepoteza imani na Marefa!!”
Licha ya kuwalaumu Wachezaji wake kwa kushindwa kuugeuza umiliki wa mechi kuwa magoli, Sir Alex Ferguson amemlaumu pia Refa Martin Atkinson kwa kuwapa Chelsea frikiki iliyozua goli bila rafu kutendeka, kwa kukubali goli hilo huku Drogba akimuangusha Wes Brown na wakati huo huo mpira kuguswa na Anelka aliekuwa ofsaidi na kuingia wavuni ingawa Chelsea wanaficha kuwa Mfungaji si Anelka na kung’ang’ania Terry ndie aliefunga.
“Ni uamuzi mbovu!” Ferguson amelalamika. “Lakini utafanyaje? Unapoteza imani kwa Marefa! Wachezaji wote wanasema Refa hakututendea haki!”
Mbali ya goli hilo kukubalika, Man U wanadhani walionewa pale dakika ya 14 Valencia alipoangushwa na Terry kwenye boksi na Refa hakutoa penalti.
Na ikafuata Rooney kupewa pande tamu na akiwa akienda kumuona Kipa Cech, kwa mshangao, ikaamuliwa ni ofsaidi.
Lakini, juu ya yote, hakuna Mdau wa Man U anaeshangaa maamuzi ya Marefa kwa kipindi hiki ambacho Wadau hao wanadai Man U inaandamwa.

No comments:

Powered By Blogger