England v Brazil
Doha, Qatar
Jumamosi, Novemba 14, Brazil na England, Mataifa yenye historia kubwa ya Soka yatacheza Doha, Qatar Uwanja wa Khalifa [pichani] wenye uwezo wa kuingiza Watazamaji 50,000.


Hapa, nje ya Uwanja wa Khalifa, kuna ‘Kijiji cha Soka’ambacho kitawakaribisha Mashabiki wanaokuja kuona pambano hilo.
Kijiji hicho cha Soka kimegawanywa mara mbili. Kuna Kijiji cha Brazil ambacho kina mfano wa Bichi maarufu huko Brazil iitwayo Copcabana na kina Kiwanja kidogo cha kuchezea Soka ya Bichi. Pia ipo Bendi iitwayo Batucada inayopiga muziki wa Brazil.
Kijiji cha England kina ile saa kubwa na maarufu Mjini London, Big Ben. Kuna ukuta mkubwa wa kuchezea ile gemu ya video, Playstation na pia yapo mashindano ya kupiga mpira danadana.
Wale Askari ambao ni kivutio kikubwa huko England kwenye Jumba la Malkia, Buckingham Palace, pia wapo. Muziki unaangushwa na Bendi toka England iitwayo Bootleg Beatles.

Imeripotiwa kuwa Hoteli zote za hapa zimejaa na wageni wametoka kila kona ya huku Arabuni toka Nchi kama Saudi Arabia, Bahrain, Kuwait, Oman na UAE.
Pia wapo washabiki kutoka England.
Brazil na England zimewahi kukutana mara 22 na Brazil kushinda mara 10 na England mara 3.
No comments:
Post a Comment