Thursday 12 November 2009

Kipa Cudicini apata ajali ya Pikipiki, aumia vibaya!!!
Kipa wa Tottenham, Carlo Cudicini, miaka 36, amepata ajali baada ya Pikipiki yake kugongana na Gari Ford Fiesta leo asubuhi na inasemekana amevunjika mikono yote miwili na pia kuumia kiuno.
Habari za ajali hiyo zimethibitishwa na Klabu yake Tottenham ambayo imesema yuko hospitalini na itawapa Washabiki taarifa zaidi hapo baadae.
Cudicini alihamia Tottenham kutoka Chelsea alikokaa kwa miaka 10 na kabla aliwahi kuzichezea Klabu za Italia AC Milan na Lazio.
Baba yake Mzazi, Fabio, alikuwa Kipa wa wa AC Milan katika miaka ya 1960.
Kindumbwendumbwe cha Misri na Algeria kitarudiwa Sudan endapo Mshindi hapatikani Jumamosi hii!!
FIFA imetangaza kuwa endapo mechi kati ya Misri na Algeria ambayo itachezwa Cairo, Misri Jumamosi hii ili kupata Timu moja itakayoenda Fainali Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwakani itashindwa kutoa Mshindi, basi mechi hiyo itarudiwa Novemba 18 huko Sudan.
Algeria na Misri wako Kundi moja na Algeria anaongoza akiwa na pointi 13 na Misri ni wa pili akiwa na pointi 10.
Ili Misri kumpiku Algeria na kwenda Fainali ni lazima ashinde 3-0 lakini mechi ikiisha kwa ushindi wa 2-0 kwa Misri basi Timu hizo zitalingana kila kitu, yaani pointi na magoli, na hivyo itabidi ichezwe uwanja nyutro ambao FIFA umeamua ni Sudan.
Matokeo mengine yeyote yataipa ushindi Algeria.
FIFA iliipa kila Nchi chagua lake la uwanja wa nyutro na Ageria ikachagua Tunisia na Misri ikachagua Sudan na ndipo ikapigwa kura ambayo Misri walishinda.

No comments:

Powered By Blogger