Friday 13 November 2009

Chama cha Marefa chadokeza kinaweza kumshitaki Fergie!!
Alan Heighton, Katibu wa Chama cha Kutetea Haki za Marefa, amedokeza kuwa wanaweza kumshitaki Sir Alex Ferguson Mahakamani kwa kumkashifu Refa Alan Wiley kwa matamshi yake kuwa Refa huyo hayuko fiti kuchezesha mechi.
Jana Kamati ya Sheria ya FA ilimtia hatiani Ferguson na kumfungia mechi 4 na kumpiga faini Pauni 20,000 lakini atatumukia kifungo cha mechi 2 tu na 2 zimwekwa kiporo hadi mwisho wa msimu wa 2010/11 ili kuchunga mwenendo wake.
Ferguson hatoruhusiwa kukaa kwenye benchi la akiba kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Novemba 21 dhidi ya Everton itakayochezwa Old Trafford na ile ya wiki inayofuatia ya Portsmouth ambayo Man U watakuwa ugenini.
Alan Heighton amesema ataongea na Refa Alan Wiley ili watoe uamuzi kama watafungua mashitaka au la.
Mwenyewe Ferguson hajazungumza lolote kuhusu adhabu hiyo ya FA na inaaminika hatakata rufaa kuipinga adhabu hiyo.
Ferguson anatakiwa awasilishe rufaa leo na mwisho ni saa 2 usiku saa za bongo.
MAMENEJA WALIODUNGWA FAINI ZA JUU:
• £200,000, ILIPUNGUZWA HADI £75,000 Jose Mourinho, Chelsea (2005) : Kwa kumrubuni Mchezaji wa Arsenal Ashley Cole.
• £20,000 Graeme Souness, Newcastle (2005): Kwa kumponda Refa wa mechi dhidi na Everton.
• £15,000 Graeme Souness, Blackburn (2005) : Alitolewa nje ya Uwanja kwenye mechi dhidi ya Liverpool.
• £15,000 Arsène Wenger, Arsenal (2004) : Kwa kauli yake kuhusu Ruud van Nistelrooy, Mchezaji wa Man U.
FAINI ALIZOWAHI KUPIGWA Ferguson:
• £10,000 NA KUFUNGIWA MECHI 2 (2008): Kumponda Refa Mike Dean aliechezesha mechi Man U v Hull.
• £10,000 (2003): Kumtukana Refa kwenye mechi ya Man U v Newcastle.
• £5,000 (2003, na Uefa): Aliposema UEFA imefiksi mechi ya Robo Fainali Man U wakutane na Real Madrid.
• £2,000 (1999,na Uefa):Kwa kuponda Marefa kwenye mechi ya Man U v Inter Milan.

No comments:

Powered By Blogger