Sunday 23 August 2009

Moyes asalimu amri kmzuia Lescott asihamie Man City!!!
Bosi wa Everton David Moyes amekubali kuwa sasa hawezi tena kumzuia Beki wake Joleon Lescott kuhamia Manchester City.
Lescott, ambae kwa sasa ameondolewa kwenye Kikosi cha Kwanza cha Everton mara baada ya mechi ya kwanza ya Ligi Kuu waliyofungwa 6-1 na Arsenal kwa kile Moyes alichokiita kukosa ari, alishaandika barua rasmi kuomba kuhamia Man City.
Moyes amekiri: "Nilitaka abaki. Ni Mchezaji mzuri anaecheza nafasi nyingi za ulinzi lakini mwenyewe hataki kubaki na kabla ya mechi na Arsenal alinambia hataki kucheza mechi hiyo lakini nililazimika kumpanga kutokana na upungufu wa Walinzi na matokeo yake mnayajua!"
Benitez akiri Ubingwa mgumu msimu huu!!!
Rafa Benitez wa Liverpool amekiri kuwa msimu huu ni mgumu sana kwa Timu yeyote kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu kupita misimu mingine yote iliyopita.
Mpaka sasa Liverpool wamefungwa mechi moja ambayo ni ile ya siku ya ufunguzi walipopigwa 2-1 na Tottenham huku nao Mabingwa Watetezi Manchester United wakipoteza mechi moja katika 3 walizocheza.
Timu pekee katika Timu "Vigogo" zilizoanza vizuri ni Chelsea na Arsenal huku Tottenham wakishinda mechi zao zote mpaka sasa.
Kesho Jumatatu usiku Liverpool wanapambana na Aston Villa.
Ferguson asifia safu yake ya Ushambulizi!!!
Sir Alex Ferguson amewasifia Washambuliaji wake Wayne Rooney, Michael Owen, Dimitar Berbatov na Nani ambao wote jana walipachika mabao katika kipigo cha 5-0 Manchester United walichowashushia Wigan.
Rooney jana alifunga mabao mawili yakiwa ni bao lake la 100 na 101 tangu aanze kuvaa Jezi za Man U.
"Ni kijana mdogo na hayo ni mafanikio makubwa sana!!" Ferguson akimzungumzia Rooney. "Na Owen ni mmliaziaji hatari sana ambae amepata kutokea nchi hii!!"

No comments:

Powered By Blogger