Tuesday 25 August 2009

Liverpool yakung’utwa 3-1 nyumbani!!!
Wakiwa ndani ya Anfield, Liverpool jana usiku walionja kipigo kikali cha pili katika mechi zao tatu za Ligi Kuu baada ya kufungwa na Timu ambayo haijawahi kushinda katika mechi zao 16 zilizopita kati yao na mara ya mwisho ilipigwa 5-0 lakini safari hii Aston Villa walisimama kidete na kuisambaratisha 3-1 Liverpool ndani ya ngome yao.
Msimu wote mzima uliopita Liverpool ilipoteza mechi 2 tu lakini msimu huu katika mechi 3 tu za kwanza Liverpool washafungwa mechi 2 na ni dhahiri Meneja Rafa Benitez ameanza kuona machungu.
Balaa kwa Liverpool lilianza pale Lucas alipojifunga mwenyewe dakika ya 34 na Davies wa Aston Villa akaongeza la pili dakika ya 45.
Lakini Mshambuliaji Fernando Torres akaipatia Liverpool bao lao moja dakika ya 72 na kidogo kufufua matumaini na lakini dakika 3 tu baadae ndipo Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard alipomwangusha Nigel Reo-Cocker kwenye boksi na Ashley Young akampeleka Kipa Reina potea katika penalti na kupachika bao la tatu na kuwaua kabisa Liverpool.
Vikosi vilikuwa:
Liverpool: Reina, Johnson, Insua, Carragher, Skrtel, Gerrard, Benayoun [Babel 75], Mascherano, Lucas, [Voronin 66], Torres, Kuyt.
Aston Villa: Friedel, Davies, Shorey, Beye, Cuellar, Sidwell, Young [Heskey 80], Milner, Petrov, Reo-Cocker, Agbonlahor.
Refa: Martin Atkinson
Watazamaji: 43667

No comments:

Powered By Blogger