Hadithi ni ile ile kama yaliyowafika Manchester United juzi walipofungwa na Timu iliyopanda Daraja msimu huu Burnley bao 1-0 na pia kukosa penalti iliyopigwa na Michael Carrick na leo Everton wamefungwa bao 1-0 na pia kukosa penalti iliyopigwa na Mchezaji wa zamani wa Manchester United Luis Saha alieutoa nje mkwaju huo wa penalti.
Kama ilivyo kwenye mechi na Manchester United, Everton walitawala kabisa huku wakikosa nafasi nyingi tu na kuwaacha Burnley wakipachika bao lao la ushindi kupitia kwa Wade Elliott dakika ya 34.
Everton mpaka sasa wamecheza mechi 2 na kufungwa zote wakati Burnley wamecheza 3 na kufungwa 1 na kushinda 2.
Tottenham yashinda mechi ya 3 mfululizo: West Ham 1 Tottenham 2
Inasemekana ni zaidi ya miaka 50 tangu mara ya mwisho kwa Tottenham kuanza msimu wa Ligi na kushinda mechi zao zote 3 za kwanza na leo wameshinda mechi yao ya 3 wakiwa ugenini baada ya kuifunga West Ham mabao 2-1.
Walikuwa ni West Ham waliopata bao la kwanza kupitia Carlton Cole aliefumua shuti kali.
Lakini dakika 5 baadae Carlton Cole akageuka kuwa mbaya pale alipotoa pasi ya kijinga kwa 'adui' Defoe ambae hakungoja kutoa shukrani bali akaisawazishia Timu yake.
Katika dakika ya 79 Winga Aaaron Lennon akaipa Tottenham bao la pili na la ushindi.
No comments:
Post a Comment