Monday 24 August 2009

Liverpool v Aston Villa
Leo, wakiwa nyumbani Anfield, Liverpool wanaikaribisha Aston Villa Klabu ambayo haijawahi kuifunga Liverpool katika mechi 16 za mwisho walizocheza kati yao.

Mechi ya mwisho kati ya Timu hizi ilikuwa ile ya Machi 22, 2009 wakati Liverpool ilipoilipua Villa mabao 5-0.
Msimu huu Aston Villa wamecheza mechi moja tu ya Ligi Kuu na kubugizwa bao 2-0 nyumbani kwao na Timu ya Wigan. Mechi iliyofuata kwa Aston Villa ilikuwa ni ile ya mtoano wa EUROPA LEAGUE ambayo nayo walifungwa 1-0 na Rapid Vienna.
Liverpool wameshacheza mechi mbili za Ligi Kuu na ya kwanza walifungwa na Tottenham 2-1 huko London na ya pili wakicheza kwao Anfield walishinda 4-0 dhidi ya Stoke City.
Refa katika mechi ya leo itakayoanza saa 4 usiku saa za bongo ni Martin Atkinson.

No comments:

Powered By Blogger