Monday, 24 August 2009

Everton wakubali ada ya Lescott toka Man City
Manchester City na Everton hatimaye zimefikia makubaliano juu ya kuuzwa kwa Beki wa Everton Joleon Lescott, umri miaka 26, baada ya vuta ni kuvute.
Ada ya uhamisho haikutajwa ila inaaminika ni Pauni Milioni 24 na Lescott atathibitishwa kuwa Mchezaji wa Man City baada ya kufaulu upimaji wa afya yake na kufikia makubaliano na Klabu yake hiyo mpya juu ya marupurupu yake.
Tovuti ya Everton ilitoa tamko: “Uamuzi huu ni bora kwa Everton. Baada ya Manchester City kuonyesha nia ya kumnunua Joleon Lescott tabia, mwenendo na ari yake vilibadilika mno.”
Man City awali ilitaka kumchukua Nahodha wa Chelsea John Terry lakini iliposhindikana wakatoa ofa ya Pauni Milioni 15 kumnunua Lescott ambae pia huchezea Timu ya Taifa ya England.
Ofa hiyo ikaongezwa hadi Pauni Milioni 18 lakini Meneja wa Everton David Moyes akang’ang’ania Lescott hauzwi.
Wiki mbili zilizopita Lescott akawasilisha ombi lake rasmi la kutaka kuhama.
Baada ya kuichezea Everton katika kipigo cha bao 6-1 na Arsenal, Moyes akambwaga Mchezaji huyo kwenye Kikosi cha Pili akidai ari yake imepungua.
Kwa sasa, Everton ambayo imeshafungwa mechi zake zote mbili za Ligi Kuu England, inabaki na Sentahafu mmoja tu na nae ni Mnigeria Joseph Yobo kwani Sentahafu wao mwingine wa kutegemewa Phil Jagielka ni majeruhi wa muda mrefu.
Wawili mbaroni kwa kumchoma visu Mchezaji wa West Ham
Polisi jijini London inawashikilia watu wawili kwa kumchoma visu Beki wa West Ham Calum Davenport, umri miaka 26, na Mama yake mzazi wakiwa nyumbani kwao Ijumaa usiku.
Hali ya Mchezaji huyo imeelezwa kuwa ni mbaya na ilibidi afanyiwe upasuaji.
Hali ya Mama yake pia ni mbaya ingawa Madaktari wameridhi
shwa nayo.

No comments:

Powered By Blogger