Mechi ya KOMBE LA CARLING: Man City v Arsenal, Van Persie ataka kisasi!!!
Ingawa kawaida Meneja Arsene Wenger hutumia Vijana Chipukizi ili kuwapa uzoefu kwenye mechi za Kombe la Carling, mara baada ya kugundua kuwa Arsenal wamepangiwa Manchester City Robin Van Persie ameonyesha shauku kubwa ya kutaka kucheza mechi hiyo ili alipe kisasi.
Van Persie aligundua Arsenal wamepangiwa Man City mara baada ya mechi ya Arsenal na Tottenham ya Ligi Kuu siku ya Jumamosi ambayo Arsenal walishinda 3-0 na yeye Van Persie kufunga bao 2.
Mara baada ya mechi hiyo, Van Persie aliuliza: “Droo ya Carling vipi? Ni Man City? Nataka kucheza!”
Usongo wa Van Persie na mechi hiyo na Man City umekuja hasa baada ya Arsenal kufungwa 4-2 na Timu hiyo kwenye mechi ya Ligi Kuu ambayo Mchezaji mwenzake wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Adebayor, ambae sasa anachezea Man City kumtimba kwa makusudi, kosa ambalo lilimfanya afungiwe mechi 3 na FA ingawa Refa hakuona kitendo hicho.
Adebayor vilevile alipigwa faini kwa kitendo chake cha kuwakebehi Mashabiki wa Arsenal alipokwenda kushangilia mbele yao mara baada ya kuifungia Man City bao katika mechi hiyo hiyo.
Van Persie amekuwa akidai kitendo cha Adebayor kilikuwa cha makusudi na kibaya sana.
Fergie awaomba Mashabiki wa Man U waache nyimbo za kashfa kwa Wenger
Arsene Wenger hukumbwa na nyimbo za Mashabiki za kumkejeli kila Uwanja wa ugenini anaoenda kucheza na Timu yake Arsenal lakini aendapo Old Trafford, nyumbani kwa Manchester United, hukumbana na nyimbo za kashfa na mojawapo ikiwa ile inayomtuhumu kubaka watoto wadogo.
Hali hiyo imemkera Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, na sasa ameamua kuandika barua ya wazi kwa Mashabiki hao wanaoimba nyimbo hizo ili waache tabia hiyo.
Ferguson pia amewataka Walinzi wa Uwanjani wa Old Trafford pamoja na Polisi kuchunguza ili kuwabaini viongozi wanaohamasisha nyimbo hizo ili wapigwe marufuku kuingia uwanjani na vile vile kushitakiwa.
No comments:
Post a Comment