ZE BIGI MECHI Jumapili: Chelsea v Man U!!!!
Refa aliewahi ‘kuiua’ Man U kuchezesha!!!!
Martin Atkinson [pichani] ameteuliwa kuchezesha mechi ya Ligi Kuu Jumapili Novemba 8 Uwanjani Stamford Bridge kati ya vinara wa Ligi Kuu Chelsea na Mabingwa Watetezi Manchester United ambao wako nafasi ya pili.Mwezi Machi 2008, Sir Alex Ferguson alipewa onyo kali na FA baada ya kumlaumu sana Refa Martin Atkinson pamoja na Kiongozi Mkuu wa Marefa, Keith Hackett, baada ya Man U kufungwa 1-0 na Portsmouth kwenye mechi ya Nusu Fainali Kombe la FA.
Katika mechi hiyo Refa Atkinson aliwanyima Man U penalti ya wazi kisha kuwapa Portsmouth penalti waliyopatia bao lao la ushindi na papo hapo kumtoa Kipa wa Man U Tomasz Kuszczak kwa Kadi Nyekundu.
Kwa wakati huu, kwa kauli yake kuhusu Refa Alan Wiley, Sir Alex Ferguson anakabiliwa na kesi huko FA.

No comments:
Post a Comment