Wednesday 4 November 2009

FA yaitupa Rufaa ya Liverpool ya Kadi Nyekundu kwa Degen, ya Carragher uamuzi bado!!!
Chama cha Soka England, FA, wameitupilia mbali Rufaa ya Liverpool waliyokata kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa Mchezaji wao Philipp Degen katika mechi ya Ligi Kuu Jumamosi iliyopita ambayo walichapwa 3-1 na Fulham.
Degen alipewa moja kwa moja Kadi Nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya Clint Dempsey na sasa atatumikia kifungo cha mechi 3 za huko England.
Liverpool pia wamekata Rufaa kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa Mchezaji wao Jamie Carragher katika mechi hiyo hiyo ya Jumamosi waliyofungwa na Fulham ambayo Carragher akiwa ndie mtu wa mwisho kwenye ulinzi alimkamata Fowadi wa Fulham Bobby Zamora na hivyo kulambwa Nyekundu.
FA haijatoa uamuzi kuhusu rufaa ya Carragher.

No comments:

Powered By Blogger