Wednesday 4 November 2009

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: Tathmini Mechi za Leo!
Arsenal bado wamo, Liverpool hatihati!!!
RATIBA:
Jumatano, 4 Novemba 2009
[saa 4 dak 45 usiku]
KUNDI E
Fiorentina v Debrecen,
Lyon v Liverpool,
KUNDI F
Rubin Kazan v Barcelona,
Dynamo Kiev v Inter Milan,
KUNDI G
Sevilla v VfB Stuttgart,
Unirea Urziceni v Rangers
KUNDI H
Arsenal v AZ Alkmaar,
Standard Liege v Olympiakos


Arsenal v AZ Alkmaar
Arsenal wakiwa nyumbani Emirates Stadium watamkosa fulbeki Gael Clichy ambae amegundulika amevunjika kimfupa cha mgongo na atakuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili.
Lakini Kiungo toka Czech Tomas Rosicky amerudi kundini baada ya kupona goti ila Mafowadi Nicklas Bendtner na Theo Walcott, Kipa Lukas Fabianski (paja) na Kiungo Denilson (mgongo) bado ni majeruhi.
Arsenal wakiwafunga AZ Alkmaar na Standard Liege washindwe kuifunga Olympiakos Arsenal watasonga mbele na kuungana na Chelsea na Manchester United Raundi inayofuata ya Mtoano ya Timu 16.
Mpaka sasa Arsenal wako kileleni Kundi H wakiwa na pointi 7 kutoka mechi 3 baada ya kushinda 2 na kutoka 1-1 na AZ Alkmaar mechi iliyokwisha.
Lyon v Liverpool
Liverpool leo wako ugenini huko Ufaransa kucheza na Lyon Timu ambayo iliifunga Liverpool mechi iliyokwisha iliyochezwa Anfield kwa bao 2-1 na leo lazima Liverpool washinde ili kufufua uhai wao wa kusonga mbele.
Endapo Liverpool watafungwa basi atabaki na matumaini finyu mno ya kufuzu kuingia Raundi inayofuata.
Mpaka sasa Liverpool wanaweweseka baada ya kufungwa mechi 6 katika 7 za mwisho walizocheza na hali hiyo haiwapi matumaini hasa kwa vile pia wanakabiliwa na majeruhi kibao.
Majeruhi hao ni Nahodha Steven Gerrard (nyonga), Albert Riera (paja), Martin Kelly (enka), Martin Skrtel (musuli na kuugua maradhi), Glen Johnson (musuli) na Fabio Aurelio (musuli).
Fernando Torres yupo Kikosini ingawa inasemekana hayuko fiti kabisa lakini atacheza.
Pia Mchezaji mpya, Alberto Aquilani huenda akachezeshwa baada ya kupona.
Katika Kundi lao Liverpool wako nafasi ya 3 huku Lyon wakiongoza wakiwa na pointi 9, Fiorentina wa pili pointi 6 na Liverpool pointi 3.
Leo Fiorentina wako nyumbani wanacheza na Vibonde wa Kundi hili Timu ambayo waliifunga mechi iliyopita kwao, Debrecen ya Hungary.

No comments:

Powered By Blogger