Saturday 18 September 2010

Sunderland 1 Arsenal 1
Darren Bent alifunga dakika ya 94 na kuifanya Timu yake Sunderland watoke droo 1-1 na Arsenal ambao walicheza takriban dakika 30 za mwisho wakiwa Mtu 10 baada ya Alex Song kupewa Kadi ya Njano ya pili na hivyo kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
Arsenal walipata bao lao kibahati tu kwenye dakika ya 12 wakati Difenda wa Sunderland Antony Ferdinand, akiwa Mita kama 30 nje ya goli lake, alipopiga mpira mbele na kumgonga Cesc Fabregas mguuni wakati akija kwa kasi kumkaba na mpira huo ukapaa juu na kumpita Kipa Mignolet aliekuwa ametoka golini.
Ukweli ni kuwa hilo goli litaingia kwenye kumbukumbu kama moja ya magoli ya ajabu na bahati kubwa.
Arsenal wangeweza kujihakikishia ushindi kwenye mechi hii lakini walikosa kufunga penalti waliyopewa kwenye dakika ya 73 baada ya Beki Mmisri wa Sunderland Ahmed Almohamady kumchezea rafu Samir Nasri na penalti iliyopigwa na Tomas Rosicky kuota mbawa.
Vikosi vilivyoanza:
Sunderland: Mignolet, Onuoha, Bramble, Ferdinand, Richardson, Elmohamady, Riveros, Meyler, Malbranque, Welbeck, Bent.
Akiba: Carson, Bardsley, Zenden, Da Silva, Reid, Colback, Gyan.
Arsenal: Almunia, Clichy, Squillaci, Koscielny, Sagna, Song, Wilshere, Nasri, Fabregas, Arshavin, Chamakh.
Akiba: Fabianski, Rosicky, Vela, Denilson, Djourou, Eboue, Gibbs.
Refa: Phil Dowd

No comments:

Powered By Blogger