Sunday 12 September 2010

Birmingham 0 Liverpool 0
Liverpool inabidi wamshukuru Kipa Pepe Reina kwa kufuta mabao ya wazi kadhaa wa kadha na kuwafanya waibuke na sare ya 0-0 ugenini na Birmingham.
Hii ni mechi ya 17 ya Ligi Kuu kwa Birmingham kutoipoteza kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Mtakatifu Andrew.
Inaelekea leo Reina alikuwa na kazi moja tu ya kuwafanya Washabiki wasahau makosa yake ya mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu alipowapa Arsenal bao la zawadi kwenye dakika za majeruhi na kuifanya mechi iwe 1-1.
Pia Reina hivi majuzi alifanya kosa la kibwege alipoidakia Nchi yake Spain na kupigwa 4-1 na Argentina.
Jumapili ijayo Septemba 19 Liverpool watatembelea Old Trafford kucheza na watani wao wa jadi Manchester United kwenye mechi ya Ligi Kuu.

No comments:

Powered By Blogger