Friday 17 September 2010

EUROPA LIGI: Liverpool & Man City zapeta, Juve droo!
Hapo jana, kwenye mechi za kwanza za Makundi yao, Manchester City, ikicheza ugenini huko Austria, iliichapa Red Bull Salzburg 2-0 na Liverpool ikiwa nyumbani Anfield iliichapa Steau Bucharest 4-1.
Juventus, Vigogo wa Italia, walishikwa koo na na Timu ‘ndogo’ kutoka Poland Lech Poznan kwa bao 3-3.
‘Timu Tajiri’ Man City ilifunga mabao yake kupitia David Silva, likiwa bao lake la kwanza kwa Klabu hiyo tangu ahamie kutoka Valencia na la pili lilifungwa na Mbrazil Jo.
Nae Joe Cole, aliifungia Liverpool bao la kwanza, na hilo likiwa bao lake la kwanza tangu ajiunge nayo, tena liliweka historia kwa kufungwa haraka mno pale lilipotinga sekunde 25 tu tangu mpira uanze.
Cristian Tanase wa Steau Bucharest alisawazisha lakini Liverpool, waliocheza bila Nyota Steven Gerrard na Fernando Torres, wakaongeza bao 3 zaidi zikifungwa na David Ngog , bao mbili, na Lucas.

No comments:

Powered By Blogger