Saturday, 18 September 2010

PITIA PITIA TOVUTI ITAKAYOTOKA UPYAAAA HIVI KARIBUNIIII: www.sokainbongo.com

BIGI MECHI: Man United v Liverpool
Jumapili, Septemba 19,
Uwanja: Old Trafford,
Saa: 9.30 mchana Bongo Taimu
TATHMINI:
Vikosi vinatarajiwa:
Manchester United (Fomesheni 4-4-1-1): Van der Sar; Neville, Vidic, Evans, Evra; Nani, Scholes, Fletcher, Park; Berbatov; Rooney
Liverpool (4-2-3-1): Reina; Johnson, Skrtel, Carragher, Konchesky; Poulsen, Meireles; Maxi, Gerrard, Jovanovic; Torres.
Refa: Howard Webb.
Historia:
Katika Mechi 18 za Ligi Kuu za Watani hawa wa Jadi Uwanjani Old Trafford, Manchester United wameshinda 10 na kupoteza 4 huku wakifunga bao 27 na kufungwa 15.
Rekodi hii ni pamoja na ushindi wa Mechi 5 katika 6 za mwisho kati yao Uwanjani Old Trafford.
Katika historia yao kwa Mechi zote 77 za Ligi zilizochezwa Old Trafford, Manchestet United wameshinda Mechi 37 na Liverpool wameshinda 15 tu huku Man United wakishindilia jumla ya mabao 127 na kufungwa 70 katika mechi zote hizo.
Meneja wa Liverpool, Roy Hodgson, awali akiwa Fulham, ashakutana na Sir Alex Ferguson wa Manchester United kwenye Mechi za Ligi Kuu mara 9 na ameweza kushinda mbili tu.
Msimu huu, Liverpool imeshinda Mechi moja tu ya Ligi Kuu, kutoka sare 2 na kufungwa 1 wakati Man United wameshinda 2 na sare 2.
Ingawa Man United walibadilisha Kikosi chao Wachezaji 10 kwenye Mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI waliyotoka droo 0-0 na Rangers Jumanne iliyopita, kesho wanategemewa kuwarudisha Wachezaji wengi waliocheza kwenye sare ya 3-3 na Everton Jumamosi iliyopita akiwemo Wayne Rooney ambae hakucheza mechi hiyo ingawa alicheza na Rangers.
Lakini, Man United itawakosa Antonio Valencia, Owen Hargreaves na Michael Carrick ambao ni majeruhi.
Liverpool itawakosa Fabio Aurelio na Dirk Kuyt.
Nini wanasema:
Sir Alex Ferguson: “Pengine naonekana kama kasuku lakini hii ni BIGI MECHI! Hamna kipingamizi kuhusu hilo! Hilo halibadiliki!”
Roy Hodgson: “Ni gemu ngumu lakini ni gemu inayovutia Dunia nzima Miaka yote hii na tuombe isiwe tofauti Wikiendi hii!”
Matokeo Msimu uliokwisha:
-Liverpool 2 Man United 0
-Man United 2 Liverpool 1
Takwimu ya Mechi:
Liverpool wameshinda mara moja katika mechi zao 11 za ugenini zilizokwisha na kufunga bao 8 tu katika Mechi 14 za mwisho.

No comments:

Powered By Blogger