Monday 13 September 2010

FA yamfungulia mashitaka Moyes
David Moyes huenda akalikwaa rungu la FA kwa kuvamia uwanja na kumvaa Refa Martin Atkinson kwa maneno mara baada ya mechi kati ya Everton na Manchester United kwisha akidai Refa huyo alipaswa
kuongeza muda katika mechi ambayo Timu yake Everton ilipata bao mbili kwenye dakika za majeruhi na kutoka sare 3-3 hapo Jumamosi katika mechi ya hiyo Ligi Kuu.
FA imeamua kumfungulia mashitaka Meneja huyo pamoja na Msaidizi wake Steve Round.
Mara baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa na Refa Martin Atkinson, Moyes alivamia uwanja na kwenda kumpa maneno yake Refa huyo kwa kile alichodai Refa hakuongeza muda ilivyopaswa.
Moyes anadai wakati Everton wanafunga mabao yao mawili dakika za majeruhi huku tayari bango lilikwisha onyesha dakika 3 za nyongeza, Refa huyo alipaswa kuongeza muda zaidi kufidia muda uliopotezwa baada ya magoli kufungwa na mpira kuanza tena.
Rooney kilingeni tena!
Straika Wayne Rooney ameendelea na mazoezi na Timu yake Manchester United hivi leo licha ya Magazeti huko Uingereza kuchapisha kila ya aina ya stori huku mengine yakidai Meneja wake amemwadhibu na ndio maana aliachwa kwenye Kikosi kilichocheza na Everton kwenye mechi ya Ligi Kuu hapo Jumamosi.
Rooney amekuwa akikabiliwa na skandali baada ya kulipuliwa kwenye baadhi ya Magazeti akidaiwa kutembea na Changudoa wakati Mkewe akiwa na mimba.
Lakini, leo Rooney alionekana mazoezini na Timu yake akiwa na wenzake huku akiwa mwenye furaha kubwa na Sir Alex Ferguson amethibitisha Rooney atacheza kesho katika mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI Old Trafford dhidi ya Rangers.

No comments:

Powered By Blogger