Saturday 2 October 2010

LIGI KUU England:
Sunderland 0 Man United 0
Huko Stadium of Light, kwenye mechi ya Ligi Kuu iliyochelewa kuanza kwa dakika 20 baada ya dari la Chumba cha Kubadilishia jezi cha Man United kuporomoka kufuatia kupasuka bomba la maji, Sunderland walicheza vizuri na kuweza kutoka sare 0-0 na Manchester United ambayo, kama kawaida ya Sir Alex Ferguson siku hizi, Kikosi kilipanguliwa na hivyo kushindwa kucheza mpira wenye mtiririko.
Kipindi cha kwanza Sunderland walitawala na walipaswa kuwa mbele kwa nafasi walizozipata.
Kipindi cha pili, Man United walizinduka alipobadilishwa Michael Owen na kuingizwa Dimitar Berbatov na wangeweza kupata bao kwa mabadiliko hayo.
Vikosi vilivyoanza:
Sunderland: Mignolet, Onuoha, Turner, Bramble, Bardsley, Malbranque, Cattermole, Henderson, Zenden, Bent, Elmohamady.
Akiba: Gordon, Mensah, Da Silva, Riveros, Reid, Ferdinand, Gyan.
Man Utd: Van der Sar, Rafael Da Silva, Ferdinand, Vidic, O'Shea, Nani, Scholes, Fletcher, Anderson, Macheda, Owen.
Akiba: Kuszczak, Evra, Berbatov, Smalling, Hernandez, Gibson, Bebe.
Refa: Chris Foy
Birmingham 0 Everton 2
Walikuwa hawajafungwa Mwaka mzima na katika mechi 18 kwenye Uwanja wao wa Mtakatifu Andrew, lakini leo Birmigham wameonja joto ya jiwe baada ya Everton kuwatandika 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu na huu ukiwa ushindi wa kwanza wa Ligi kwao.
Everton waliandika bao la kwanza baada ya krosi ya Leon Osman kumkuta Roger Johnson aliejifunga mwenyewe.
Krosi ya Leighton Barnes ilimkuta Tim Cahill na kufunga kwa kichwa bao la pili.
MATOKEO Mechi nyingine:
Stoke 1 Blackburn 0
Tottenham 2 Aston Villa 1
West Brom 1 Bolton 1
West Ham 1 Fulham 1
RATIBA KESHO:
Jumapili, 3 Octoba 2010
[Saa 9 na nusu mchana]
Man City v Newcastle
[Saa 11 jioni]
Liverpool v Blackpool
[Saa 12 jioni]
Chelsea v Arsenal

No comments:

Powered By Blogger