Tuesday 28 September 2010

Rooney nje Wiki 3
Manchester United imetangaza kuwa Wayne Rooney hatacheza kwa wiki 3 ili kuuguza enka yake aliyoumia Jumamosi kwenye mechi ya Ligi Kuu walipocheza na Bolton na kutoka sare 2-2.
Rooney hakuwemo kwenye Kikosi cha Man United kilichoenda Spain kucheza na Valencia hapo kesho kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI .
Pia Nyota huyo atazikosa mechi ya Ligi Kuu ya Jumamosi Man United watakapoenda ugenini kucheza na Sunderland na pia mechi ya England ya EURO 2012 dhidi ya Montenegro Oktoba 12.
Mbali ya kuumia, fomu ya Rooney Msimu huu imeporomoka na hata Meneja wake wa Man United Sir Alex Ferguson amekiri hilo na kusema ni kwa sababu ya kusakamwa mno na Magazeti.
Hivi karibuni, Rooney alilipuliwa na Magazeti na skandali la kudaiwa kutembea na changudoa wakati mkewe akiwa mja mzito.
FA yamshitaki Meneja wa Blackpool
Meneja wa Blackpool Ian Holloway ameshitakiwa kwa utovu wa nidhamu na vitendo vyake kwa Marefa.
Jumamosi, Blackpool, wakiwa nyumbani, walifungwa 2-1 na Blackburn kwenye mechi ya Ligi Kuu na Holloway alichukizwa na goli la pili kufungwa kwenye dakika za majeruhi.
Baada ya mechi, Holloway alitamka: “Refa [Mike Dean] alichezesha vibaya na najua ataniripoti kwa kumpa maneno yake baada ya mechi wakati tukitoka uwanjani. Nadhani kulikuwa na maamuzi ya kushangaza.”
Blackpool waliudhiwa na goli la ushindi la Blackburn kufungwa dakika za majeruhi huku Mfungaji Brett Emerton akiwa ofsaidi na pia wakati linaenda kufungwa Mchezaji wa Blackpool, Gary Taylor-Fletcher, alifanyiwa madhambi.
Kufuatia na kanuni mpya za FA za kuharakisha kesi, Holloway anatakiwa ajibu mashitaka hayo ifikapo Ijumaa na akikiri kabla ya hapo atapigwa Faini ya Pauni 8000 na kufungiwa mechi moja.
Ikiwa atapinga mashitaka yake kesi itapelekwa kwenye Kamati ya Sheria na huko anaweza kupewa adhabu kali zaidi akipatikana na hatia.

No comments:

Powered By Blogger