Friday 1 October 2010

Wenger: ‘Arsenal ya kuungaunga ina uwezo kuifunga Chelsea!’
Arsene Wenger ana imani kubwa Timu yake Arsenal inao uwezo mkubwa kuwafunga Mabingwa Watetezi na vinara wa Ligi Kuu, Chelsea, watakapokutana Jumapili huko Stamford Bridge licha ya kuwakosa Wachezaji kadhaa wa Timu ya kwanza.
Siku hiyo, Arsenal itabidi icheze bila Nahodha Cesc Fabregas na Mastaa wengine kama vile Kipa Manuel Almunia, Kieran Gibbs, Thomas Vermaelen, Theo Walcott na Robin van Persie ambao wote ni majeruhi.
Arsenal walifungwa 3-2 na West Brom kwenye mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu wikiendi iliyopita Uwanjani Emirates lakini juzi walishinda kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI huko Serbia kwa kuilaza Partizan Belgrade 3-1.
Wenger amedai: “Naamini tuna uwezo wa kushinda. Tukicheza vizuri tutashinda. Uwezo upo licha ya Chelsea kuwa Timu nzuri.”
Spurs yahofia Huddlestone kufungiwa na UEFA!
Klabu ya Tottenham Hotspur inasubiri kwa wasiwasi mkubwa uchunguzi wa UEFA kuhusu Mchezaji wao Tom Huddlestone ambae alionekana akimpiga kiwiko Mchezaji wa FC Twente Marc Janko kwenye mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI Jumatano huko White Hart Lane ambayo Spurs walishinda bao 4-1.
Janko amedai Huddlestone alikusudia kumpiga kipepsi wakati Wachezaji hao walipovaana katika tukio ambalo Refa alipiga filimbi kuashiria ni Janko ndie aliecheza faulo.
UEFA imethibitisha kuchunguza mikanda ya tukio hilo na endapo Huddlestone atapatikana na hatia atafungiwa mechi zijazo za Tottenham za UEFA CHAMPIONS LIGI ambazo ni pamoja na mechi mbili mfululizo na Inter Milan.

No comments:

Powered By Blogger