Scholes & Rooney nje tripu ya Spain
Manchester United imeelekea Spain ambako kesho itacheza na Vinara wa La Liga Valencia kwenye mechi ya Kundi lao ya UEFA CHAMPIONS LIGI bila ya Wachezaji mahiri kadhaa kwenye Kikosi cha Wachezaji 22.
Paul Scholes, Wayne Rooney na Ryan Giggs hawakwenda Spain na wakati Scholes amepumzishwa tu, Rooney na Giggs ni majeruhi.
Lakini Kiungo Michael Carrick ambae hajacheza tangu mechi ya ufunguzi ya Msimu huu ya Ngao ya Hisani dhidi ya Chelsea yumo baada ya kupona maumivu na huenda kesho akacheza.
Katika mechi za ufunguzi za Kundi C, Man United walitoka sare 0-0 na Rangers wakati Valencia waliichapa ugenini Bursapor ya Uturuki kwa bao 4-0.
Licha ya kuondokewa na Mastaa wao David Villa na David Silva, Valencia ndio wametwaa uongozi wa La Liga Msimu huu na Kiungo wa Man United Darren Fletcher amekiri: “Ni mechi ngumu. Wao wameanza vizuri Ligi yao lakini sisi wazoefu wa mechi za Ulaya.”
Fletcher ameongeza pia kwa kusema kitu muhimu ukicheza na Timu za Spain ni kumiliki mpira kwani ukiupoteza utachukua muda mrefu kuunasa tena na hilo litakutesa.
Kikosi kilichosafiri ni:
Van der Sar, Kuszczak, Amos, Rafael, O'Shea, Brown, Ferdinand, Vidic, Evans, Smalling, Evra, Nani, Fletcher, Anderson, Carrick, Gibson, Park, Bebe, Berbatov, Owen, Hernandez, Macheda.
No comments:
Post a Comment