Sunday 26 September 2010

Newcastle 1 Stoke 2
Bao la kujifunga mwenyewe la Beki James Perch la dakika ya 85 leo limewapa ushindi Stoke City wa 2-1 dhidi ya Newcastle wakiwa ugenini St James Park kwenye mechi ya Ligi Kuu.
Newcastle walitangulia kupata bao dakika ya 45 kwa penati ya Kevin Nolan lakini Stoke wakarudisha KIpindi cha Pili dakika ya 67 Mfungaji akiwa Kenwyne Jones.
Wolves 1 Aston Villa 2
Bao la kichwa la Emile Heskey dakika ya 88 limempa Meneja mpya wa Aston Villa Gerard Houllier ushindi wake wa kwanza walipocheza Ligi Kuu Uwanja wa Molineux leo na wenyeji Wolves.
Stewart Downing ndie aliwapa Villa bao la kwanza dakika ya 25 na Kipindi cha Pili Wolves walisawazisha dakika ya 62 kupitia Mathew Jarvis.
Ushindi huu umewafanya Villa wafikishe pointi 10 na kudandia nafasi ya 5.
LIGI KUU ENGLAND: Mechi zijazo
Jumamosi, 2 Octoba 2010
[Saa za Bongo]
[Saa 8 dak 45 mchana]
Wigan v Wolverhampton
[Saa 11 jioni]
Birmingham v Everton
Stoke v Blackburn
Sunderland v Man United
Tottenham v Aston Villa
West Brom v Bolton
West Ham v Fulham
Jumapili, 3 Octoba 2010
[Saa 9 na nusu mchana]
Man City v Newcastle
[Saa 11 jioni]
Liverpool v Blackpool
[Saa 12 jioni]
Chelsea v Arsenal
Wenger alalama na Ze Gunners yake!!
Arsene Wenger ameiponda Timu yake Arsenal kufuatia kubondwa jana kwenye mechi ya Ligi Kuu na West Bromwich Albion ambao walijikuta wapo 3-0 mbele kwa mabao ya Peter Odemwingie, Gonzalo Jara na Jerome Thomas lakini Samir Nasri akaifungia Arsenal bao mbili na kufanya mechi imalizike 3-2.
Wenger ametamka” “Ni uchezaji mbovu kwenye difensi na mbele. Hakuna hata Mchezaji mmoja aliecheza kiwango!”
Jumapili ijayo Oktoba 3 kwenye mechi ya Ligi Kuu, Arsenal wataitembelea Stamford Bridge kupambana na Chelsea ambao pia hapo jana walichapwa 1-0 na Manchester City.
Wenger alikataa kumnyooshea kidole Kipa Manuel Almunia ingawa alikuwa mmoja wa Wachezaji waliocheza ovyo kwa kusababisha penati ingawa aliiokoa lakini baadae akafungwa bao mbili ambazo Wataalam wanadai ni makosa yake.
Wakati Wenger ananung’unika, Bosi wa West Brom, Roberto Di Matteo, ameipongeza Timu yake na kudai ilistahili kushinda.

No comments:

Powered By Blogger