UEFA CHAMPIONS LIGI: Vumbi Ulaya kesho na Jumatano
Ratiba
Jumanne, 28 Septemba 2010
[Saa 3 dak 45 usiku bongo taimu]
Spartak Moscow v MSK Zilina [Saa 1 na nusu usiku]
Ajax v AC Milan
Auxerre v Real Madrid
Basle v Bayern Munich
Braga v Shakhtar Donetsk
Chelsea v Marseille
Partizan Belgrade v Arsenal
Roma v CFR 1907 Cluj-Napoca
________________________________________
Jumatano, 29 Septemba 2010
[Saa 3 dak 45 usiku bongo taimu]
Rubin Kazan v Barcelona [Saa 1 na nusu usiku]
Hapoel Tel-Aviv v Lyon
Inter Milan v Werder Bremen
Panathinaikos v FC Copenhagen
Rangers v Bursaspor
Schalke 04 v Benfica
Tottenham v FC Twente
Valencia v Man Utd
Tathmini:
Mabingwa Inter Milan, Washindi wa Pili Bayern Munich, wanaoshikilia rekodi ya Ubingwa Ulaya mara nyingi Real Madrid na Klabu za England nne, Chelsea, Manchester United, Tottenham na Arsenal, zote zilipata matokeo yasiyoridhisha kwenye Ligi za nyumbani kwao Wikiendi hii.
Kati ya Vigogo hao 7 wa Ulaya, hakuna alieshinda mechi zao za Ligi huku Inter, Bayern, Chelsea, Arsenal na Tottenham Hotspur wakifungwa na Real Madrid na Manchester United wakipata sare.
Sasa Vigogo hao 7 watalenga makucha yao huko Ulaya kesho Jumanne na kesho kutwa Jumatano kuwania ushindi katika mechi za pili za Makundi yao katika kinyang’anyiro cha UEFA CHAMPIONS LIGI.
Katika Kundi H, Arsenal wanasafiri kwenda kuikumba Partizan Belgrade wakitokea kwenye ushindi wa 6-0 dhidi ya Sporting Braga katika mechi yao ya kwanza ya Kundi lao.
Kwenye mechi hii ya kesho, Arsenal inakabiliwa na majeruhi wakiwemo Kipa Manuel Almunia, Cesc Fabregas, Abou Diaby, Robin van Persie, Theo Walcott, Nicklas Bendtner, Kieran Gibbs na Thomas Vermaelen.
Mabingwa wa England Chelsea, waliopigwa 1-0 na Manchester City Jumamosi kwenye Ligi Kuu, wanawakaribisha Wafaransa Olympique Marseille Uwanjani Stamford Bridge Siku ya Jumanne.
Chelsea inao majeruhi kwa Mastaa wao wakiwemo Frank Lampard, Salomon Kalou na Yossi Benayoun na huku Didier Drogba akiwa amesimamishwa kwa mechi hii.
Chelsea walishinda mechi yao ya kwanza huko Slovakia kwa kuifunga MSK Zilina 4-1.
Jumanne, Bayern Munich watakuwa Uswisi kucheza na Basel huku wakitokea kwenye kipigo cha 2-1 kwenye Bundesliga dhidi ya Mainz.
Kocha wa Basel ni Thorsten Fink ambae aliwahi kutwaa Ubingwa wa Ulaya wakati akiwa Mchezaji wa Bayern Munich Mwaka 2001.
Kundi G ni mechi kati ya Auxerre na Real Madrid na Ajax Amsterdam v AC Milan.
Mabingwa Watetezi Inter Milan watakuwa nyumbani kucheza na Werder Bremen na hii ni mechi muhimu kwao baada ya kuanza utetezi wa taji lao kwa sare ya 2-2 na Mabingwa wa Uholanzi FC Twente Enschede.
Katika mechi nyingine ya Kundi hili la Inter Milan, Tottenham watacheza na FC Twente.
Manchester United, waliotoka sare 0-0 na Rangers, watatua Metsalla Stadium kucheza na vinara wa La Liga Valencia bila Nyota wao Wayne Rooney, Mkongwe Ryan Giggs na Winga Luis Antonio Valencia kwani wote ni majeruhi.
Rangers watakuwa nyumbani kucheza na Waturuki Bursapor.
No comments:
Post a Comment