Monday 27 September 2010

Kipa Almunia nje UEFA CHAMPIONS LIGI
Manuel Almunia ataikosa tripu ya mechi ya UEFA Champions Ligi kwenda kucheza na Partizan Belgrade Siku ya Jumanne baada ya kuumia kiwiko cha mkono kwenye mechi ya Ligi Kuu Jumamosi Arsenal walipofungwa 3-2 na West Bromwich Albion Uwanjani Emirates.
Almunia aliumia wakati alipomwangusha Mshambuliaji wa West Bromwich Peter Odemwingie na kusababisha penati ambayo ilipigwa na Chris Brunt lakini aliikoa.
Hata hivyo Almunia aliingia lawamani kwa kushindwa kuzuia bao rahisi la pili baada ya shuti la Gonzalo Jara kumpenya lakini Meneja wake Arsene Wenger amekataa kumnyooshea kidole.
Kipa wa akiba Lukasz Fabianski anategemewa kudaka katika mechi hiyo na Partizan Belgrade.
Ruud amtaka Rooney ajali Soka lake tu
Ruud van Nistelrooy amemtaka Wayne Rooney kupuuza Magazeti yanayomsakama na badala yake atilie mkazo Soka tu.
Hivi karibuni Magazeti yalimlipua Rooney kwa kutembea na changudoa na hata Meneja wake wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amesema kuandamwa huko kumechangia kushuka kwa kiwango chake.
Lakini Ruud van Nistelrooy, Mchezaji wa zamani wa Manchester United, amemtaka Rooney kupuuza Magazeti hayo na amesema: “Ni England pekee Magazeti yanakusama kuhusu maisha yako ya faragha.”

No comments:

Powered By Blogger