Sunday, 24 August 2008

TUZO WACHEZAJI BORA WA KLABU ULAYA KUTOLEWA ALHAMISI 28 AGOSTI 2008!!!!
-ratiba ya KLABU BINGWA ULAYA kutolewa siku hiyo!!!
-MCHEZAJI BORA WA KLABU ULAYA KUJULIKANA siku hiyo!!!
-MAN U KUGOMBEA UEFA SUPER CUP siku inayofuata!!!!

Chama cha Mpira ULAYA, UEFA, siku ya Alhamisi tarehe 28 Agosti 2008, kitatangaza washindi wa tuzo mbalimbali za Wachezaji Bora wa Klabu za Ulaya kwa msimu wa 2007/8 na vilevile siku hiyo hiyo itafanyika droo maalum ili kupanga Makundi ya Mashindano ya LIGI ya KLABU BINGWA ULAYA ya msimu huu 2008/9 ambayo itaanza tarehe 16 Septemba 2008.
Siku inayofuata, yaani tarehe 29 Agosti 2008, Mabingwa wa LIGI ya KLABU BINGWA ULAYA Manchester United watapambana na Mabingwa wa Kombe la UEFA Zenit St Petersburg ya Urusi kugombea UEFA Super Cup mjini Monaco kwenye Uwanja wa Stade Louis II.
Kati ya Wachezaji 20 waliomo kwenye listi ya mwisho ya Wachezaji Bora, wachezaji 17 wanatoka kwenye Klabu za LIGI KUU UINGEREZA.
Hii inadhihirisha ubora wa LIGI KUU UINGEREZA katika Ulaya na Dunia.
Wachezaji 6 wanatoka kwa Mabingwa wa Ulaya Manchester United, watano Chelsea, wanne Liverpool na wawil Arsenal. Wachezaji wengine watatu waliobaki ni Kipa wa Schalke 04 Manuel Neuer, Mlinzi wa Barcelona Carles Puyol na Mchezaji mwenzake wa Barcelona Mshambuliaji Lionel Messi.
Majina ya Wachezaji wa Manchester United ni Edwin van der Sar, Rio Ferdinand, Nemanja Vidic, Paul Scholes, Wayne Rooney na Cristiano Ronaldo.
Wa Chelsea ni Peter Cech, John Terry, Michael Essien, Frank Lampard, Didier Drogba. Liverpool ni Pepe Reina, Jamie Carragher, Steven Gerrard na Fernando Torres. Arsenal ni Manuel Almunia na Cesc Fabregas.
Kila Mchezaji atakuwa anagombea nafasi Bora katika pozisheni anayochezea yaani kama ni Kipa basi Kipa Bora, Mlinzi zawadi ya Mlinzi Bora, Kiungo zawadi ya Kiungo Bora na Mshambuliaji tuzo ya Mshambuliaji Bora.
Juu ya yote, mmoja kati ya hawa Wachezaji 20 Bora ndie atakaevikwa Taji la Mchezaji Bora wa Klabu Ulaya kwa msimu wa 2007/8.
Wachezaji hawa 20 waliteuliwa kwa kupigiwa kura na Makocha wa Klabu 16 za Ulaya zilizoingia hatua ya mtoano ya Mashindano ya LIGI ya KLABU BINGWA ULAYA
ya msimu uliopita.

No comments:

Powered By Blogger