Wednesday 27 August 2008

UHAMISHO LIGI KUU:
-Mdogo wake Rio njiani kwenda Sunderland, Senderos safarini AC Milan, Berbatov bado kanasa!!!
Wakati mdogo wake Rio Ferdinand, sentahafu wa West Ham Anton Ferdinand [23] akifanyiwa uchunguzi wa afya ili kukamilisha taratibu za kuhamia Sunderland na sentahafu wa Arsenal Philippe Senderos nae pia akipimwa afya ili ahamie kwa mkopo AC Milan, Dimitar Berbatov amekwama kuhamia Manchester United baada ya Klabu yake Tottenham Hotspurs kung’ang’ania waongezewe dau.
Mvutano huo umefikia hatua ya kuzorotesha uhusiano kati ya Berbatov na Tottenham kiasi cha klabu hiyo kumtema katika kikosi chake kilichofungwa na Sunderland wikiendi kwa bao 2-1.
Mchezaji huyo ameshadai kwa maandishi ili aruhusiwe kuhamia Man United.
Tayari Man U washatoa ofa mbili rasmi zilizokataliwa na Tottenham wanaotaka dau liwe Pauni milioni 30 wakati ofa waliyopewa ni Pauni milioni 25.
Tarehe ya mwisho ya kukamilisha usajili ni Jumatatu Septemba 1 na baada ya hapo mchezaji haruhusiwi kuhama hadi Januari 1, 2009.

No comments:

Powered By Blogger