Saturday 2 January 2010

Wenger kubadili Timu FA Cup
Bosi wa Arsenal Arsene Wenger amesema atabadili Kikosi chake kitakachocheza na West Ham kwenye Kombe la FA hapo kesho na kuwapumzisha Mastaa wake kwa ajili ya mechi zijazo za Ligi Kuu dhidi ya Bolton Jumatano ijayo na Everton wikiendi ijayo.
Wenger ametamka: “Baadhi ya Wachezaji watapumzika. Tunataka kushinda lakini kwetu Ligi Kuu ni muhimu kuliko FA Cup!”
Arsenal haijatwaa Kikombe chochote tangu mwaka 2005.
Mbrazil Jo asimamishwa Everton kwa kwenda kula Xmas kwao!!!
Everton imemsimamisha kwa muda usiojulikana Mshambuliaji Jo kutoka Brazil ambae yuko hapo kwa mkopo akitokea Manchester City kwa sababu aliondoka Klabuni bila ruhusa na kwenda kula Sikukuu ya Xmas kwao Brazil.
Meneja wa Everton David Moyes amesema: “Tunampenda Jo lakini Klabu ina taratibu zake. Aliondoka bila ruhusa. Tumemsimamisha!”
Jo, miaka 22, ambae jina lake kamili ni Joao Alves de Assis Silva, alinunuliwa na Man City kutoka CSKA Moscow Julai 2008 kwa Pauni Milioni 18 lakini akakosa namba na ndipo akakopeshwa kwa Everton ambako nako pia mara nyingi huwekwa benchi la akiba.

No comments:

Powered By Blogger