Wednesday 7 May 2008


WIGAN ITAPATA DONGE NONO IKIIFUNGA MAN U!!!!


WAKATI LIGI KUU UINGEREZA INATEGEMEWA KUFIKA MWISHO JUMAPILI HII HUKU CHELSEA WAKIOMBA MUNGU MAN UNITED WATELEZE KATIKA MECHI YAO NA WIGAN, WACHEZAJI NA MENEJA WA CHELSEA WAMEONEKA 'WAKIIBEMBELEZA WIGAN IIWEKEE NGUMU MAN U.

ENDAPO MAN U ATAIFUNGA TU WIGAN BASI UBINGWA UNAENDA OLD TRAFFORD!!!

NAE MENEJA WA WIGAN, STEVE BRUCE [ALIEKUWA MCHEZAJI WA ZAMANI WA MAN U] AMEJARIBU KUONDOA UTATA KWAMBA WIGAN 'ITAACHIA' KWA KUSEMA KUWA WIGAN WANACHANGAMOTO KUBWA KATIKA KUSHINDA MECHI HIYO INGAWA KWA SASA WAMESHAPONA BALAA LA KUSHUKA DARAJA.

STEVE BRUCE ALISEMA: 'SISI TUPO NAFASI YA 13 KATIKA MSIMAMO WA LIGI NA ENDAPO TUTAIFUNGA MAN U NA EVERTON WATAIFUNGA NEWCASTLE BASI TUTAMALIZA KATIKA NAFASI YA 12 NA HIVYO KUSHINDA PAUNI ZA UINGEREZA MILIONI 6 LAKI 4 LAKINI TUKIFUNGWA NA MAN U TUTAMALIZA TUKIWA NAFASI YA 15 NA HIVYO KUPATA MILIONI 4 LAKI 3 TU, HASARA YA PAUNI MILIONI 2 LAKI 1!!! SASA NANI ANADAI HATUNA SABABU YA KUSHINDA?'

No comments:

Powered By Blogger