Monday 5 May 2008


WEST BROMWICH ALBION NA STOKE CITY ZAPANDA DARAJA KUINGIA LIGI KUU UINGEREZA!!!!


TIMU ZA WEST BROMWICH ALBION NA STOKE CITY ZIMEINGIA LIGI KUU UINGEREZA BAADA YA KUSHIKA NAFASI MBILI ZA KWANZA KATIKA LIGI IITWAYO COCA COLA FOOTBALL LEAGUE CHAMPIONSHIP SIKU YA JUMAPILI.


West Bromwich wamechukua UBINGWA na STOKE CITY ilishika nafasi ya pili.


Timu ya tatu itakayoungana nao kupanda daraja itaamuliwa katika mtoano utaohusisha timu za HULL, BRISTOL CITY, CRYSTAL PALACE na WATFORD.

==============================================================


HUKO SPAIN, TIMU YA REAL MADRID IMETWAA UBINGWA WA LA LIGA SPAIN HUKU ZIKIWA ZIMEBAKI MECHI TATU.

REAL waliwafunga OSASUNA 2-1 na walicheza watu 10 katika mechi hiyo baada ya mchezaji wao, FABIO CANNAVARO, kutolewa kwa kadi nyekundu.


==============================================================


LIGI KUU UINGEREZA KUFIKA TAMATI JUMAPILI TAREHE 11 MEI 2008!!!


Timu zote [isipokuwa CHELSEA na NEWCASTLE wanaocheza leo JUMATATU saa 12 jioni] zimebakiza mechi moja ambazo zitachezwa JUMAPILI HII SAA 11 jioni.

Wakati Ubingwa utakuwa wa MAN U au CHELSEA, na tayari DERBY imeshashuka daraja [kuzipisha WEST BROMWICH na STOKE CITY zilizopanda daraja], timu nyingine mbili zitakazoungana na DERBY zitakuwa ama BIRMINGHAM au READING au FULHAM au BOLTON [ingawa BOLTON nafasi yake kushuka ni finyu sana!].


MATOKEO YA MECHI ZA JUMAMOSI NA JUMAPILI NI:

JUMAPILI

ARSENAL 1 EVERTON O [BENDTNER 77]

LIVERPOOL 1 MAN CITY 0 [TORRES]


JUMAMOSI

ASTON VILLA 0 WIGAN 2

BLACKBURN 3 DERBY 1

BOLTON 2 SUNDERLAND 0

FULHAM 2 BIRMINGHAM 0

MAN U 4 WEST HAM 1

BORO 2 PORTSMOUTH 0

READING 0 SPURS 1



No comments:

Powered By Blogger