Masupastaa wa Soka kufunzwa kuendesha Magari!!! Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa kutoa mafunzo hayo!!!!
PFA, Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa England, kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wake, Gordon Taylor, kimetangaza mpango kamambe wa kuwafundisha Mastaa wote wa Soka jinsi ya kuendesha magari kwa ustadi zaidi kufuatia wimbi la ajali na mikasa kadhaa inayowakumba Mastaa hao wakiwa kwenye magari yao ya bei mbaya, yenye nguvu sana na kasi za ajabu.
Hivi majuzi tu, Cristiano Ronaldo alinusurika na kuliteketeza gari lake la bei mbaya sana la aina ya Ferrari pale alipopata ajali akiwa kwenye mwendo wa kasi mjini Manchester.
Nae Mchezaji mwenzake wa Man U, Carlos Tevez, alibambwa na Polisi wa Manchester akiendesha gari huku akiwa hana Leseni ya kuendesha magari ya England.
Manchester City kuikwaa Hamburg ya Ujerumani Robo Fainali UEFA CUP
Klabu pekee ya England iliyobaki kwenye Kombe la UEFA, Manchester Ciy, imepangiwa kukutana na Hamburg ya Ujerumani kwenye Robo Fainali Kombe la UEFA.
Ikishinda mechi hiyo itapambana na Mshindi kati ya Werder Bremen au Udinese kwenye Nusu Fainali.
Ratiba kamili ya UEFA CUP ni:
ROBO FAINALI [mechi kuchezwa Aprili 9 na marudiano Aprili 16]
Hamburg v Manchester City
Paris St Germain [PSG] v Dynamo Kiev
Shakhtar Donetsk v Marseille
Werder Bremen v Udinese
NUSU FAINALI [kuchezwa Aprili 30 na marudio Mei 7]
Werder Bremen/Udinese v Hamburg/Man City
PSG/Dynamo Kiev v Shakhtar Donetsk/Marseille
Drogba aonywa na Polisi!!!
Mchezaji wa Chelsea anaetoka Ivory Coast, Didier Drogba, ameepuka kuburuzwa Mahakamani na badala yake kupewa onyo kali baada ya kuwarushia Mashabiki wa Burnley sarafu mara baada ya kufunga goli kwenye mechi kati ya Chelsea na Burnley kugombea Kombe la Carling iliyochezwa Novemba mwaka jana na kumalizika 1-1 lakini Chelsea wakatolewa kwa penalti tano tano.
FA ilimfungia Drogba mechi 3 kwa kitendo hicho.
Polisi baada ya uchunguzi na kushauriana na Waendesha Mashtaka waliamua kumwita Makao Makuu na kumpa onyo kali badala ya kumshtaki Mahakamani.
Nae Steven Gerrard afutiwa shtaka moja Mahakamani lakini kesi kuendelea kwa shtaka moja jingine!!!
Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, amefutiwa Shtaka la kushambulia kwa kutumia nguvu lakini bado anakabiliwa na shtaka jingine la kuvunja amani na kusababisha vurugu hadharani.
Gerrard yuko kwenye kesi hiyo inaowahusisha wenzake watano kufuatia ugomvi na vurugu zilizotokea ndani ya Naiti Klabu moja huko Liverpool mnamo Desemba 29 ambako DJ wa Klabu hiyo aliumizwa usoni.
Kesi hiyo itaendelea tena Aprili 3.
No comments:
Post a Comment