Tuesday 7 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Houllier Meneja mpya Villa
Aliekuwa Meneja wa zamani wa Liverpool, Gerrard Houllier, amesaini Mkataba wa Miaka miwili wa kuwa Meneja mpya wa Aston Villa kuchukua nafasi ya Martin O’Neill alieondoka mwenyewe.
Houllier, Miaka 63, amekuwa kwenye majadiliano na Villa kwa wiki moja na kesho anategemewa kutangazwa rasmi.
Houllier anategemewa kumchukua Msaidizi wake wa zamani wa Liverpool, Phil Thompson, awe tena Msaidizi wake huko Aston Villa.
Sare na Algeria yazua ndoto Bongo!
Baada ya kutoka sare na Algeria ya 1-1 Siku ya Ijumaa kwenye mechi ya Makundi kuwania kuingia Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika iliyochezwa huko Algiers, ndoto za Wadau wa Bongo za kucheza Fainali kwa mara ya kwanza tangu 1980 zimefufuka hasa baada ya Vigogo wengine, Morocco, ambao wapo Kundi moja na Tanzania, kutoka sare 0-0 na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Mechi inayofuata kwa Taifa Stars ni ya ugenini tena huko Morocco Novemba 9 na kufuatiwa na mechi ya nyumbani kucheza na Jamhuri ya Afrika ya Kati Machi Mwakani.
Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitachezwa Mwaka 2012 huko Equatorial Guinea na Gabon, kwa pamoja.

No comments:

Powered By Blogger