Monday 6 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

‘Les Bleus’ piga ua kesho!!!
Huku jahazi likiendelea kutota kufuatia aibu ya Fainali za Kombe la Dunia iliyozaa kufungiwa baadhi ya Nyota wao na kufungwa nyumbani katika mechi ya kwanza tu ya EURO 2012, kesho Ufaransa ipo ugenini kucheza na Bosnia-Herzegovina katika mechi ya pili ya Kundi lao kuwania kuingia Fainali za EURO 2012.
Siku ya Ijumaa, Les Bleus walichapwa 1-0 na Belarus na kipigo hicho kilimfanya Beki wa Ufaransa anaecheza Arsenal akiite ni ‘kupigwa kibao usoni’.
Sagna ametamka: “Tumepigwa kibao usoni lakini kesho ni siku nyingine na lazima tufanye kazi ya ziada.”
Ufaransa kwa sasa ipo chini ya Kocha mpya, Gwiji la zamani, Laurent Blanc na inawakosa Wachezaji Nyota kama Nahodha wao Patrice Evra na Franck Ribery ambao wako kifungoni kufuatia sakata la huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
………..Anelka bado MSTAAFU!!!!!!!!!!!!!
Staa wa Chelsea, Nicolas Anelka, amesisitiza msimamo wake kuwa yeye alistaafu kuichezea Ufaransa tangu Juni 19 siku aliyofukuzwa kwenye Timu hiyo ya Ufaransa huko Afrika Kusini ilipokuwa kwenye Kombe la Dunia.
Anelka, Miaka 31, amedai hamna uwezekano wowote wa kurudi kuichezea Les Bleus [maana yake Timu ya Bluu] baada ya kifungo chake cha mechi 18 alichopewa kufuatia sakata lake la huko Afrika Kusini.
Mchezaji huyo wa Chelsea ametamka: “Sina haja kuchezea Les Bleus kwani kila Wikiendi naichezea Bluu ya Chelsea!”

No comments:

Powered By Blogger