Monday 6 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Rooney yuko Uswisi na England
Licha ya kulipuliwa kwenye baadhi ya Magazeti huko Uingereza na skandali la kutembea na Changudoa na pia kudaiwa atatupwa nje ya Timu ya Taifa ya England, Wayne Rooney aliondoka na Wachezaji wenzake kwenda Uswisi ili kucheza mechi ya Kundi lao kwenye EURO 2012 ambapo kesho watacheza na Uswisi.
Magazeti hayo yamemwandama Staa huyo wa Manchester United na pia tegemeo kubwa la England huku mengine yakidai Wadhamini wake, Makampuni ya Nike, EA Sports na Coca Cola, yanafikiria kumtema.
Lakini, Kampuni ya Nike tayari imeshatangaza kuwa wataendelea kubakia na Rooney na kuwa sakata lililomkumba ni suala binafsi la Rooney na Familia yake.
Kampuni ya Nike ilikuwa na msimamo kama huo baada ya Mcheza Gofu maarufu Tiger Woods kukumbwa na skandali la ngono nje ya ndoa.
Nao Coca Cola wamefuata nyayo za Nike na kudai hilo ni suala binafsi la Rooney na Familia yake.
Nayo Magazeti mengine, pengine yakigundua kuwa kutokuwepo kwa Rooney kwenye Timu ya England ni pigo kubwa, yamemwomba Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, aingilie na kumnyoosha Rooney ili aepuke maisha mabovu na hivyo kuisaidia England ifanye vyema kwenye michuano ya Kimataifa kwa vile Mchezaji huyo ndie mkombozi wao.
Bebe yumo Kikosi cha UEFA
UEFA imethibitisha kuwa Mchezaji mpya wa Manchester United, Bebe, kutoka Ureno yumo miongoni mwa Kikosi kilichosajiliwa kwao kwa ajili ya michuano ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Kulikuwa na taarifa kwenye Vyombo vya Habari kuwa Bebe na Owen Hargreaves ndio Wachezaji ambao hakusajiliwa lakini UEFA imethibitisha ni Hargreaves tu ndie ambae hayumo kwenye Kikosi hicho cha Wachezaji 25.
Hivyo Bebe yuko huru kuichezea Man United Jumanne ijayo dhidi ya Rangers ya Scotland katika mechi ya kwanza ya Kundi lao ya UEFA CHAMPIONS LIGI.

No comments:

Powered By Blogger