Thursday 9 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com
Capello kula pensheni 2012
Fabio Capello amethibitisha ataendelea kuwa Kocha wa England hadi Mkataba wake utakapomalizika Mwaka 2012.
Mtaliana huyo aliingia madarakani Mwaka 2008 kwa Mkataba wa Miaka miwili na nusu lakini Mkataba huo ukaongezwa kabla ya kuanza kwa Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini mwezi Juni.
Baada ya kubwagwa nje Raundi ya Pili huko Afrika Kusini kwa kichapo cha 4-1 toka kwa Ujerumani, kumekuwa na manung’uniko kuwa iikuwa makosa kumwongezea Mkataba kabla ya Mashindano makubwa.
England kwa sasa imeanza kampeni ya kuingia Fainali za EURO 2012 zitakazochezwa huko Poland na Ukraine kwa pamoja Mwaka 2012 na tayari Capello, Miaka 64, ameshaiongoza England katika ushindi wa mechi mbili zao za kwanza za Kundi lao walipozichapa Bulgaria na Uswisi kwa mabao 4-0 na 3-1 kila mmoja hivi juzi.
Mechi inayofuata ya England kwenye Kundi lao ni Oktoba 12 watakapokuwa Wembley kucheza na Montenegro.
Capello ameahidi kuhakikisha England inafika Fainali za EURO 2012 lakini hataendelea kuwa Kocha baada ya hapo kwa kuwa umri wake utakuwa mkubwa na angependelea kula pensheni yake kwa raha.
Balotelli kula kisu gotini
Fowadi wa Manchester City Mario Balotelli atafanyiwa operesheni ya goti na atakuwa nje kwa Wiki 6.
Supa Mario aliumia goti kwenye mechi na FC Tmisoara ya EUROPA LIGI hapo Agosti 19 na ingawa alipumzishwa ili apate nafuu alijitonesha mazoezini Wiki iliyopita na sasa imelazimu apasuliwe.
Balotelli, Miaka 20, alihamia Man City kutoka Inter Milan kwa kitita cha Pauni Milioni 21 Mwezi uliokwisha na amechezea Man City dakika 33 tu katika mechi na FC Timisoara ambayo Man City walishinda 1-0.
Supa Mario atazikosa mechi za Klabu yake dhidi ya Chelsea kwenye Ligi Kuu na ile ya EUROPA LIGI na Juventus.
Inategemewa atarudi uwanjani kabla ya pambano la Ligi Kuu na Arsenal hapo Oktoba 24.

No comments:

Powered By Blogger