Wednesday 8 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Vilabu Ulaya vyaishukia FIFA
Chama cha Klabu za Ulaya, ECA [European Clubs Association], kimeitaka FIFA ifikirie upya katika upanganji wake wa Kalenda ya Mechi za Kimataifa za Kirafiki.
ECA, yenye Vilabu Wanachama 200 huko Ulaya zikiwemo Timu zote Vigogo, wametaka mazungumzo ya haraka na FIFA baada ya Mameneja wengi wa Klabu hizo kulalamika kuwepo kwa Mechi za Kimataifa za kirafiki Mwezi Agosti wakati wakiwa wanajitayarisha kwa Msimu mpya wa Ligi.
Mwenyekiti wa ECA, Karl-Heinz Rummenigge, ameziponda Mechi hizo na kuziita upuuzi mtupu.
Rummenigge ameitaka FIFA ielewe kuwa Klabu ndizo Waajiri wa Wachezaji na hivyo wana kila haki kuitaka FIFA ikubaliane nao.
ECA pia imeitaka FIFA na UEFA kuwakatia Bima Wachezaji ili Klabu zilipwe wakiumia wakati wanachezea Timu za Taifa.
Rufaa ya Evra kusikilizwa kesho
Rufaa ya Nahodha wa Ufaransa kupinga kifungo cha mechi 5 itasikilizwa kesho na Kamisheni ya Rufaa ya FFF, Shirikisho la Soka Ufaransa.
Patrice Evra alifungiwa mechi 5 baada ya Timu yao kugoma kufanya mazoezi hapo Juni 20 walipokuwa Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia wakipinga kufukuzwa kwa Mchezaji mwenzao Nicolas Anelka aliekuwa amegombana na Kocha wa Ufaransa wakati huo, Raymond Domenech.
Pamoja na Evra, Wachezaji wengine wa Ufaransa waliofungiwa kufuatia sakata hilo la Kombe la Dunia ni Anelka, mechi 18, Franck Ribery, mechi 3 na Jeremy Toulalan, mechi moja.

No comments:

Powered By Blogger