Tuesday 7 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Vermaelen adai Fabregas ni Barca damu!
Beki wa Arsenal, Thomas Vermaelen, amekiri kuwa Mchezaji mwenzake hapo Arsenal Cesc Fabregas ana damu ya FC Barcelona.
Fabregas amekuwa akihusishwa na kurudi tena Barca kwa muda mrefu sasa, Klabu ambayo alianza nayo Soka akiwa mtoto.
Ingawa alitegemewa kuhamia huko Barca kabla Msimu huu haujanza lakini Arsenal wakamng’ang’ania na kuikataa ofa rasmi ya Barcelona.
Vermaelen ametoboa kwa kusema: “Cesc anaibeba Barca moyoni mwake, ipo kwenye damu yake…hivyo ni ngumu yeye kuisahau Barca!”
Hivi juzi, Fabregas alikaririwa akisema kuwa Arsenal ilikataa yeye kwenda Barcelona lakini hawezi kusema nini walichoongea yeye na Meneja wake wa Arsenal Arsene Wenger.
Gibson akerwa na Kocha wa kwao Ireland
Kiungo Chipukizi wa Manchester United Darron Gibson amechukizwa na Kocha wa Timu ya Jamhuri ya Ireland, Giovanni Trapattoni, kwa kumtaka aondoke Man United ili aende Timu nyingine kupata namba ya kudumu na hivyo kuweza kuchaguliwa Kikosi cha Kwanza cha Ireland.
Gibson, Miaka 22, amekuwa hachezeshwi kwenye Timu ya Ireland na
Trapattoni na kama kawaida Ijumaa iliyopita alipigwa benchi kwenye mechi ya EURO 2012 dhidi ya Armenia waliyoshinda 1-0 na leo anategemewa tena kuwa nje kwenye mechi na Andorra ya EURO 2012.
Gibson amesema: “Kama Trapattoni anataka nihame Klabu kama Manchester United niende Timu kama Stoke ili nicheze mechi nyingi lakini nikose nafasi ya kushinda Vikombe, simuelewi! Wapi unaweza kwenda ukitoka Man United? Kwenye Klabu ipi, kama si Man United, nnakoweza kukuza kiwango?”

No comments:

Powered By Blogger