Thursday 9 September 2010

CHEKI: www.sokainbongo.com

Jagielka adai Mashabiki Everton watamzomea Rooney
Phil Jagielka amedai Wayne Rooney atapata wakati mgumu mno kutoka kwa Mashabiki wa Everton wakati Manchester United watakapoenda kucheza mechi ya Ligi Kuu huko Goodison Park siku ya Jumamosi.
Rooney aliihama Everton Mwaka 2004 kwenda kucheza Manchester United na amekuwa akizomewa kila anaporudi kucheza Uwanja wa Goodison Park na Timu yake Man United lakini safari hii Mashabiki hao wa Everton wamepata sababu ya kumzomea zaidi baada ya Staa huyo kulipuliwa na baadhi ya Magazeti kuwa alitembea na Changudoa wakati Mkewe akiwa mja mzito.
Jagielka ana hamu ya kucheza dhidi ya Rooney baada ya Jumanne kucheza Timu moja wakati wote wawili walipokuwepo kwenye Kikosi cha England kilichoifunga Uswisi 3-1 kwenye mechi ya EURO 2012.
Jagielka amesema: “Atapata shida toka kwa Mashabiki lakini Rooney ni kichwa ngumu hivyo hatasumbuka. Mie ntafurahia kushindana nae.”
Rio ategemea kuendelea Unahodha England
Rio Ferdinand anategemea kuendelea kuwa Nahodha wa England ingawa kumekuwa na mbiu kutoka baadhi ya Magazeti kuwa Unahodha apewe Steven Gerrard ambae amejizolea sifa toka Magazeti hayo kwa kile kinachodaiwa kuiongoza vyema Timu katika ushindi wa mechi mbili za EURO 2012 dhidi ya Bulgaria na Uswisi hivi majuzi.
Kocha wa England, Fabio Capello, amelipanchi suala hilo kwa kutamka: “Kwangu uchezaji wa Mchezaji ni muhimu sana kupita nani ni Nahodha.”
Hata hivyo, Ferdinand, ambae yuko fiti baada ya kuumia goti lilimkosesha Kombe la Dunia, amedokeza kuwa ana uhakika kubaki Nahodha kwenye mechi ya EURO 2012 hapo Oktoba 12 dhidi ya Montenegro.

No comments:

Powered By Blogger